Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi mwenye (kanzu nyeupe) akiwahudumia wananchi mbalimbali waliojitokeza katika tukio la iftar aliyoiandaa kwa wadau wa mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
*****************
Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali ya Umoja wa Afrika ya Mabadiliko ya Tabianchi imeiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa kituo cha mafunzo ya vijana kuhusu masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi wakati akihutubia katika tukio la iftar maalum aliyoiandaa kwa wadau wa mazingira na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo Endelevu kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Amesema kamati hiyo imeiteua Tanzania kuwa mjumbe wa kudumu kupitia mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 14-15 Februari, 2026 na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameeleza kuwa kituo hicho kitawasaidia Watanzania hususani vijana kuweza kujifunza fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya mazingira na kuongeza kupanua wigo wa ushiriki wa Tanzania katika mijadala mbalimbali ya kimataifa.
Kwa upande wake, Balozi wa Mazingira wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Bi. Frida Amani akizungumza katika hafla hiyio amesema masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi ndio ajenda ndio kuu iliyotawala mijadala mbalimbali ya kimataifa.
Amesema kutokana na ukubwa wa mijadala hiyo, fursa mbalimbali zimeweza kuibuliwana kuwahimiza vijana kucngamkia nafasi hizo na kuhakikisha ajenda ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inaleta mabadiliko Chanya katika jamii.
“Nawahimiza vijana wenzangu tushirikiane na Serikali katika kuunga mkono juhudi za utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwani ni fursa” amesema Frida ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania (Bongo flavour).
Naye Katibu wa Taasisi ya The Green Samia, Bi. Sarah Pima amesema taasisi hiyo imeendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuhakikisha jitihada za uhifadhi na utunzaji wa mazingira zinaungwa mkono na wadau wote wa maendeleo.
Amesema taasisi hiyo imekuwa ikishiriki katika kampeni mbalimbali za utunzaji wa mazingira ikiwemo kufanya usafi katika maeneo ya fukwe za Bahari na upandaji miti hatua inayolenga kuchochea hamasa kwa jamii kutambua umuhimu wa mazingira.
Tukio hilo la iftar liliwashirikisha pia watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kutoka Kata ya Magwepande, Taasisi ya Green Samia pamoja na Walimu na Wanafunzi wa Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (mwenye kanzu) akimhudumia Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi hiyo Bi. Kemilembe Mutasa kupata iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (mwenye kanzu) akimhudumia Mbunge wa Buhigwe Mkoani Kigoma, Mhe. Prof. Pius Yanda ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kupata iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akimhudumia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma kupata iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akizungumza jambo na Mbunge wa Buhigwe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Bw. Emmanuel Mbilinyi wakati wa iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi hiyo, Bi. Kemilembe Mutasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa tukio la iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akimkabidhi zawadi Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS), Hamis Omary muda mfupi baada ya kumalizika kwa iftar aliyoiandaa mwishoni mwa wiki kwa wadau wa mazingira na kufanyika Chuoni hapoBunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akimkabidhi zawadi Mkuu wa Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS), Maria Mushi muda mfupi baada ya kumalizika kwa iftar aliyoiandaa kwa wadau wa mazingira na kufanyika Chuoni hapo mwishoni mwa wiki Bunju Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiagana na Balozi wa Mazingira wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flavour), Frida Amani mfupi baada ya kukamilika kwa tukio la iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira wa Ofisi hiyo, Bw. Kaninzio Manyika muda mfupi baada ya kukamilika kwa tukio la iftar aliyoiandaa kwa wadau mazingira mwishoni mwa wiki na kufanyika katika Chuo cha Mazingira, Mabadiliko ya tabianchi na Maendeleo Endelevu (IECDS) kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)









Social Plugin