Kila alfajiri, Mwanadamu mwenye akili timamu anapambana. Anaamka kabla ya jogoo kuwika, akijipanga kwenda kutafuta riziki ili familia yake ipate chakula, ada, na matumaini ya kesho. Lakini katika mbio hizi zisizo na pumziko, jambo moja muhimu hubaki nyuma—afya yake na ya familia yake. Na pale ugonjwa unapogonga, suluhisho la haraka huwa ni kununua dawa dukani bila ushauri wa daktari. Wengi huona ni njia ya kuokoa muda na gharama—bila kujua wanacheza na hatima ya maisha yao.
Karibu katika malaka hii inayohusu matumizi yasiyo sahihi ya dawa za hospitali na dawa za tiba ya asili, watu wengi wamekuwa wakitumia bila kupewa utaratibu na wataalamu wa afya hivyo kupelekea madhara kwenye maisha yao na hata vifo.
Na Sumai Salum
Mamlaka ya Dawa na vifaa Tiba TMDA ni taasisi ya serikali Nchini Tanzania inayoongozwa na Dkt. Adam Fimbo akiwa ndiye Mkurugenzi wake mkuu, inahusika na kusimamia usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Huku lengo lake kuu ni kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa hizi zilizosajiliwa zinafuata viwango vya kimataifa, ikijumuisha udhibiti wa dawa za binadamu na mifugo.
TMDA inazo ofisi kwenye kanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
- Kanda ya Ziwa: Mwanza
- Kanda ya Mashariki: Dar es Salaam
- Kanda ya Nyanda za Juu Kusini: Mbeya
- Kanda ya Kusini: Mtwara
- Kanda ya Magharibi: Tabora
- Kanda ya Kaskazini: Arusha
Ofisi hizi zinahudumia mikoa mbalimbali iliyoko jirani na maeneo husika kwa shughuli za usajili, ukaguzi, na udhibiti wa dawa na vifaa tiba.
Pamoja na juhudi zinazofanywa na TMDA katika kudhibiti ubora na usalama wa dawa nchini, bado matumizi yasiyo sahihi ya dawa yanaendelea kuwa tishio kwa afya ya jamii. Hali hii inaonesha kuwa, licha ya uwepo wa mifumo imara ya udhibiti, uelewa na nidhamu ya watumiaji wa dawa ni muhimu katika kuzuia madhara yanayonyemelea kimya kimya.
Hivyo taasisi hii ni muhimu, kwani TMDA inalinda umma dhidi ya dawa zisizo na ubora, ghushi, au zisizo salama, na hivyo kusaidia katika kuimarisha afya ya jamii nchini Tanzania
Simulizi ya Rebecca John mkazi wa mtaa wa Majengo Kata ya Kishapu wilayani ya Kishapu mkoani Shinyanga, ni ushuhuda mchungu wa kile kinachoweza kutokea.
“Nilikuwa nikiona mwanangu mwenye miezi saba akichemka, nanunua dawa kwenye duka la dawa bila ushauri wa daktari. Hali ilivyobadilika na kuwa mbaya, nikampeleka Hospitali ya Wilaya… kumbe nilikuwa nimechelewa.”
Mama huyo anaeleza kuwa mtoto wake mwenye umri wa miezi saba alianza kuugua kwa dalili za kawaida—homa na mafua na joto la hapa na pale mwilini mwake. Kama ilivyokuwa kawaida yake, aliamua kununua dawa katika duka la dawa la karibu bila kipimo wala ushauri wa kitaalamu. Siku zilivyopita, hali ya mtoto ilizidi kuwa mbaya.
“Niliamua kumpeleka hospitali ya Dkt. Kikwete ya Kishapu Madaktari walipambana kwa kweli kuokoa maisha ya mwanangu. Walinipokea haraka, wakaanza kumpa huduma, hata akawekewa mashine ya kumsaidia kupumua… lakini haikuwa bahati yangu. Nilimpoteza mwanangu kwa ugonjwa wa Nimonia.”
Kwa sauti ya huzuni na majuto, mama huyo anasema tukio hilo limekuwa funzo kubwa maishani mwake.“Sasa hivi, hata mtoto akiwa na mafua tu, nampeleka hospitali. Ni heri nitumie gharama kumuona daktari kuliko hasara niliyoipata ya kumpoteza mwanangu. Niliumia sana.”
Kipo kisa cha kaka mmoja aitwae Suleima mkazi wa Msalala mume wa mke mke mmoja na watoto watatu, nilikutana nae miaka kadhaa iliyopita hospitali ya Wilaya ya Kahama kijana yule aliniambia alipata ajari alipokuwa amebebwa kwenye pikipiki na kisha hakwenda hospitali kuchomwa tetenasi na matibabu mengine bali aliamu kutumia dawa za tiba ya asili.
"Nilidhani hapo napata nafuu lakini baadae mguu wangu ukaanza kutoa harufu kari kiasi cha watu kutotamani kunikaria nikamaua nije hospitalini na sasa imebainika mguu wangu umeharibika naelekea hospitali ya Nkinga mkoani tabora kwa ajili ya uchunguzi zaidi maana ndugu zangu wamenitaka twende huko" alisema
Msomaji wa makala hii juhudi zangu za kutaka kujua hali yake ilivyo ziligonga mwamba hadi wiki mbili hakuwa anapatikana na ndugu zake hawakuwa wakipokea simu zangu lakini baada ya wiki ya tatu Selemani alinipigia simu nikamuuliza unaendeleaje akaongea kwa hudhuni kuwa "Dada yangu mimi sasa nina mguu mmoja sina miwili tena nimekuwa mlemavu na familia inanitegemea" kisha akaanza kulia hiyo ni baada ya uchunguzi wa kitaalamu kubaini mguu wake tayari ulikuwa umeharibika ukakatwa.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Butuyu, Kata ya Bunambiyu, Wilaya ya Kishapu, wanaeleza sababu zinazopelekea matumizi yasiyo sahihi ya dawa ambapo Leah Emmanuel anasema hali ngumu ya kiuchumi inawalazimu watu wengi kukimbilia kununua dawa moja kwa moja badala ya kwenda hospitali.
“Watu wengi wanajua si sahihi, lakini gharama za hospitali na umbali vinawakatisha tamaa. Wanachagua njia rahisi ambayo mara nyingi ni hatari.”
Kwa upande wake, Shengu Nkanda anaongeza kuwa mila na mitazamo ya zamani bado ina mchango mkubwa.“Watu wanaamini wakinywa vidonge viwili wanapaswa kupona mara moja. Maumivu yakichelewa kuisha, wanaamini wamerogwa. Hapo ndipo wanaanza kutumia tiba za asili bila vipimo wala ushauri wengine wanawahi kufika hospitali na kupona, lakini wengine wanafariki njiani au hata wakiwa hospitalini kutokana na kuchelewa kupata huduma.”
Mwenyekiti wa tiba za asili Kishapu aeleza utaratibu wa huduma
Mwenyekiti wa tiba za asili Wilaya ya Kishapu Ndembi Mabeshi, amesema waganga wa tiba za asili wanafanya kazi kwa kufuata miongozo ya serikali licha ya taaluma yao kuwa ya jadi iliyorithiwa kutoka kwa wazee. Ameeleza kuwa huduma zao zinazingatia utaratibu maalum wa matibabu ili kuhakikisha usalama wa wagonjwa.
Amesema wataalamu hao hutoa dawa kwa kuzingatia dozi kulingana na aina ya ugonjwa, sawa na ilivyo kwa tiba za kisasa, huku wakilenga kumsaidia mgonjwa kupata nafuu bila madhara. Aidha, wanapokutana na changamoto zinazozidi uwezo wao, huwapa wagonjwa rufaa kwa wataalamu wengine au kuwaelekeza hospitalini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Mabeshi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya tiba za asili na tiba za kisasa katika kuboresha afya za wananchi. Ameongeza kuwa kufuata taratibu na miongozo ya serikali ni muhimu ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa salama na zenye tija kwa jamii.
Kauli ya wadau wa maduka ya dawa binafsi
Wauzaji wa maduka ya dawa binafsi wanakiri kuwa wanakutana na changamoto kubwa kutoka kwa wateja.
Mmiliki mmoja wa duka la dawa Grace Masangu anasema. “Wateja wengi wanakuja wakitaka dawa fulani moja kwa moja. tukijaribu kuwaelekeza waende hospitali, wengine wanakataa kwa sababu ya gharama au haraka. Wengine hata wanadai wana uzoefu wa kutumia dawa hizo.”
Anaongeza kuwa wakati mwingine, shinikizo la biashara huwafanya baadhi ya wauzaji kutofuata kikamilifu taratibu. “Tunajitahidi kufuata maadili ya taaluma, lakini ukweli ni kwamba sio wote wanaozingatia. Elimu zaidi inahitajika kwa wauzaji na wateja pia.”ameongeza Grace
Aidha amebainisha sababu nyingine ni mimba za mapema (kabla ya ndoa) na kisha mume kukwepa majukumu ya kulea ujauzito hadi mtoto na ikiwa mama huyo hana uhakika wa kipato basi hali uwa mbaya zaidi pindi mtoto ama mama anapopata shida ya kiafya
Kauli ya Kiongozi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Mhunze wilayani humo Fabiani Makongo anasema matumizi ya dawa majumbani ni kielelezo tosha cha elimu ndogo kwa jamii na si suala la uchumi, hivyo elimu inahitajika itolewe sana hasa elimu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa yasiyo sahihi na elimu ya bima ya afya kwa wote
" Wananchi wanapaswa wapewe elimu lakini pia upo mpango wa serikali ambao tunaona unalenga kuwasaiida wananchi wa kaya duni kupitia TASAF na pia sasa Kuna mpango mwingine mzuri wa Bima ya afya kwa watu wote ambao tunaona tunapunguza gharama za maisha ambapo serikali imeweke kiwango cha 150,000 Watu sita kwa Kaya moja, mwanzo utaona ni kiasi kikubwa lakini Bima hiyo inafanya kazi kubwa na kumhakikishia mteja upataji wa huduma Bora na kwa wakati wowote" ameongeza
Amesema mara nyingi wanapofanya mikutano yao ya hadhara wanaita watalamu mbalimbali wakiwemo wa afya ambapo wameona mikutano hiyo ikileta matumaini kwa waliokosa matumaini akitolea Mfano mkutano wa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi Mwaka 2025 uliozaa matunda kwa kumsaidia mwanaume mmoja aliyekosa fedha ya matibabu ya tezi dume na akachangiwa na jamii na kisha kwenda kupata matibabu na sasa ni mzima na anaendelea na shughuli zake.
Mratibu Tiba asili na Tiba mbadala
Mratibu wa tiba asili na tiba mbadala Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Lilian Waero anasema matumizi ya dawa zozote bila maelekezo ya daktari baada ya vipimo ni hatari na matumizi bila kuzingatia dozi ni kufanya mwili uwe sugu
Amesema hakuna madhara yanayotokana na kuchanganya dawa za asili na za hospital isipokuwa mgonjwa huyo hatafahamu amepona ugonjwa alipokuwa nao kwa dawa ipi.
Amesema hata waalamu wa tiba asili wanatoa dawa kwa maelekezo na kipimo maalumu na dawa za asili zilizothibitishwa na mamlaka yenye dhamana (TMDA) ndio zinaruhusiwa kuwa ndani ya hospitali na endapo daktari ataona ugonjwa wa mteja wake unafaa kutumia dawa hiyo anamuandikia na anaanza kuitumia kwa maelekezo yake ila zile zinazouzwa mitaani kiholela wananchi hawatakiwi kuziamini na kuzitumia.
Ametolea mfano wa mjamzito anapokuwa kwenye kipindi cha kujifungua hospitalini hapewi dawa zozote ila wapo ambao wanamtumia dawa za asili kwa lengo la kuongeza uchungu inapekea kizazi kupata shida na hatimaye kuvuja damu nyingi kupelekea mtoto ama mama kufariki wakati wa kujifungua na hiyo haikubaliki.
Kauli ya Mganga Mfawidhi Hospitali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Dkt. Mohamed Mkumbwa, amesema matumizi ya dawa bila uchunguzi wa kitabibu na ufuatiliaji wa wataalamu husababisha vimelea kuzoea dawa, na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa uwezo wa dawa hizo kufanya kazi.
“Matumizi ya antibiotics yanapaswa kufuata mwongozo wa kitabibu unaozingatia aina ya ugonjwa, kiwango chake na majibu ya ugonjwa. Kutotimiza dozi au kutumia dawa bila ushauri wa daktari huongeza uwezekano wa vimelea kuwa sugu,” amesema Dkt. Mkumbwa.
Tafiti zinaonyesha kwamba usugu wa dawa ni miongoni mwa changamoto kubwa za afya ya umma duniani, ukichangiwa na matumizi mabaya ya antibiotics kwa binadamu. maambukizi ambayo hapo awali yalikuwa yanatibika yanaweza kuwa magumu au yasiyotibika kabisa kwa dawa hizo.
Mbali na usugu wa dawa, matumizi holela yanaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja mwilini, ikiwa ni pamoja na sumu (toxicity), mzio (allergic reactions), na uharibifu wa viungo muhimu kama ini na figo. Watoto wachanga wako katika hatari zaidi kutokana na mifumo yao ya mwili ambayo bado haijakomaa kikamilifu.
Dkt. Mkumbwa ameongeza kuwa kuna hatari ya mwingiliano wa dawa (drug interactions), hasa pale dawa za hospitali zinapochanganywa na dawa za asili zisizo na uthibitisho wa kisayansi, hali inayoweza kupunguza ufanisi wa matibabu au kuongeza sumu mwilini.
Wataalamu wa afya wanasisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya dawa kwa kufuata kanuni za kitaalamu, ikiwemo kufanya uchunguzi kabla ya tiba, kufuata dozi kamili, na kuepuka kujitibu binafsi.
Jitihada za serikali kukabiliana na tatizo
Serikali kupitia Wizara ya Afya na TMDA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya dawa kwenye jamii. Aidha, kampeni za uhamasishaji zimekuwa zikisisitiza umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kutumia dawa yoyote.

Bima ya afya kwa watu wote
Kwa upande wake, Mratibu wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita, amesema kuwa mpango huo ni suluhisho muhimu kwa wananchi katika kukabiliana na gharama za matibabu zisizotarajiwa. Amebainisha kuwa licha ya baadhi ya wananchi kuona kiwango cha mchango kuwa kikubwa mwanzoni, manufaa yake ni makubwa na ya muda mrefu.
“Bima ya afya kwa wote inalenga kumkinga mwananchi dhidi ya mzigo wa gharama za matibabu na kumhakikishia huduma bora wakati wowote anapohitaji. Tunatoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiunga na kunufaika na mpango huu wa serikali,” amesema Mwita
Matumizi yasiyo sahihi ya dawa si tu yanahatarisha afya—bali yanagharimu maisha. Simulizi ya mama wa Majengo na kijana Selemani ni kengele kwa jamii nzima. Katika harakati za kutafuta riziki, ni rahisi kusahau kwamba afya ndiyo msingi wa kila kitu. Bila afya, hata hiyo riziki haina maana.
Ni wakati wa kubadilika. Ni wakati wa kuchagua usalama badala ya haraka. Ni wakati wa kuthamini maisha. Kwa sababu wakati mwingine, kuchelewa kidogo hospitalini kunaweza kuwepo na tofauti ndogo kati ya uhai na kifo.

Leah Emmanuel mkazi wa Kijiji cha Butuyu Kata ya Bunambiyu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga

Shengu Nkanda mkazi wa Kijiji cha Butuyu Kata ya Bunambiyu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga

Mmiliki na muuzaji wa duka la dawa binafsi Grace Masangu

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Mhunze wilayani Kishapu Fabiani Makongo
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Dkt. Mohamed Mkumbwa

Mratibu wa Bima ya afya mkoani wa Shinyanga, Moses Mwita

Social Plugin