Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

GEN'Z WAJIFUNZE AMANI ILIVYOSAIDIA USTAWI NA MAENDELEO YA NCHI- MANG'ATI



Na mwandishi wetu,Dar

Vijana wa Kata ya Pugu, Wilayani Ilala Mkoani Dar Es Salaam wamehimizwa kusoma na kuijua Historia ya Tanzania na hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa nchini, msingi ukitajwa kuwa amani, utulivu na usalama unaoshuhudiwa kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Frank Mang'ati, Diwani wa Kata ya Pugu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa amani kwa maendeleo na ustawi wa wananchi, akibainisha pia wajibu wake mkubwa katika kuhakikisha amani inaendelea kutawala katika eneo lake la kiungozi.

"Mimi kama kama Kiongozi nawajibika kuhakikisha amani inakuwepo Pugu na huwezi kuongoza vyema kama amani hiyo hakuna. Amani ndio tunu ya Taifa letu na tunapaswa kuijali na kuienzi kwani amani na Utanzania wetu ndio inayotuunganisha." Amesisitiza Mhe. Mang'ati.

"Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, tunao wajibu wa kuhakikisha nchi yetu inastawi na kushamiri katika amani. Wito wangu kwa Vijana almaarufu kama GenZ, Tujifunze tujue Taifa letu lilipotoka, lilipo na tunapokwenda na namna amani ilivyotusaidia katika ustawi na maendeleo ya nchi yetu." Ameongeza kusema Mhe. Mang'ati.

Akibainisha jukumu la kila raia katika kulinda utu wa Mtanzania, amani na Utaifa, Kiongozi huyo amesema amani ndio imekuwa msingi wa maendeleo ya Tanzania kwa muda wote, akitaka kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani inaendelea kushamiri nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com