Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MISA TANZANIA WASHUHUDIA VIVUTIO IRINGA, WANAHABARI WAASWA KUWA MABALOZI WA UTALII

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Waandishi wa habari na wahariri kutoka maeneo mbalimbali nchini wametembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa, kwa lengo la kuvitangaza na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia utalii wa ndani.

Ziara hiyo ya Machi 18,2026 imefanyika sambamba na kongamano la MISA TAN Summit 2026, lililowakutanisha wadau wa habari kujadili fursa za maendeleo na nafasi ya vyombo vya habari katika kukuza sekta ya utalii.

VIVUTIO WALIVYOTEMBELEA IRINGA

Katika ziara hiyo, wanahabari walipata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vyenye historia na uzuri wa kipekee.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Isimila Stone Age Site, eneo lenye umuhimu mkubwa kihistoria likiwa na mabaki ya zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale pamoja na nguzo za mchanga zilizoundwa kwa maelfu ya miaka.

Pia walitembelea Gangilonga Rock, jiwe maarufu lenye historia ya asili ya Wahehe na linalotoa mandhari ya kuvutia ya mji wa Iringa, pamoja na Chief Mkwawa Memorial Site, eneo la kumbukumbu ya Chifu Mkwawa linaloelezea historia ya mapambano dhidi ya ukoloni.

Aidha, walifika katika Forestry and Wood Industries Training Centre (FWITC), kituo cha mafunzo kinachohusu misitu na viwanda vya mbao ambacho pia ni kivutio kwa wanaopenda masuala ya uhifadhi wa mazingira.

Ziara hiyo pia iliwapeleka katika Sao Hill Forest Plantation, moja ya mashamba makubwa ya miti barani Afrika, yanayovutia kwa uzuri wake wa asili na mchango wake katika uchumi, pamoja na Iringa Boma, jengo la kihistoria la enzi za ukoloni wa Kijerumani linalotumika kama makumbusho ya historia ya mji huo.


Akizungumza Machi 17, 2026 wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema mkoa huo una nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha utalii katika Kanda ya Kusini kutokana na wingi wa vivutio vyake.

Ametaja vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Ruaha National Park, Milima ya Udzungwa, pamoja na maeneo ya kihistoria kama Isimila na Kalenga, na mashamba ya miti ya Sao Hill.

Kwa upande wao, washiriki wa kongamano hilo wamesema ziara hiyo imewapa uelewa mpana kuhusu rasilimali za utalii zilizopo nchini na namna zinavyoweza kutangazwa kwa ufanisi.

Wamesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kubadili mtazamo wa jamii kwa kuandaa maudhui yatakayohamasisha Watanzania kushiriki utalii wa ndani.

Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema lengo ni kuwajengea wanahabari uwezo wa kuwa mabalozi wa kuitangaza Tanzania kupitia kazi zao.

Amesema kupitia kalamu na vyombo vya habari, wanahabari wana nafasi ya kipekee ya kuhamasisha jamii kutembelea vivutio vya utalii na hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Ameongeza kuwa sekta ya utalii ni moja ya nguzo kuu za uchumi wa taifa, hivyo kuitangaza kwa nguvu kupitia vyombo vya habari kutasaidia kuongeza idadi ya watalii na kukuza uchumi wa maeneo mbalimbali nchini.






MISA TANZANIA WAFANYA UTALII WA NDANI IRINGA KUTANGAZA VIVUTIO








Na Marco Maduhu, IRINGA








Wahariri na waandishi wa habari wanaoshiriki kongamano la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA Tanzania) wamepata fursa ya kufanya utalii wa ndani mkoani Iringa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.




Ziara hiyo imefanyika leo Machi 18, 2026 ikiwa ni sehemu ya siku ya pili ya kongamano la MISA TAN Summit 2026, ambapo washiriki walitembelea hifadhi mbalimbali kujionea vivutio vya utalii ikiwamo Makumbusho ya Chifu Mkwawa.








Akizungumza kuhusu ziara hiyo Mwenyekiti wa Misa Tanzania Edwin Soko, amesema, lengo ni kuwafanya waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kutangaza vivutio vya utalii wa ndani, kwa kutumia kalamu na vyombo vya habari kuhamasisha Watanzania kutembelea maeneo ya vivutio hivyo.








Amesema Iringa ni miongoni mwa mikoa yenye fursa kubwa za utalii, zikiwemo hifadhi za taifa, mandhari ya kuvutia na urithi wa kihistoria, hivyo kuna umuhimu wa vyombo vya habari kusaidia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com