Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AUNGANA NA VIONGOZI MBALIMBALI KWENYE MISA YA KUMUAGA KARDINALI PENGO



Na mwandishi wetu,Dar es Salaam,

Leo Februari 27, 2026 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki pamoja na viongozi mbalimbali katika Misa Takatifu ya kumuombea na kumuaga Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Jijini Dar es Salaam.

Wananchi walioshiriki Misa hiyo wamesema kuwa mchango wa Kardinali Pengo utaendelea kuishi kupitia miradi ya kijamii, malezi ya vijana na uongozi wa kidini alioutoa kwa moyo mkunjufu.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com