KAYA 2,257 KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE- DC KISHAPU
Friday, February 27, 2026
Na Sumai Salum- Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi, leo Februari 27,2026 amezindua rasmi mpango wa Bima ya Afya kwa watu wote wilayani humo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya michezo vya Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu.
Uzinduzi huo umeenda sambamba na uhamasishaji mkubwa kwa wananchi kujiunga na mpango huo muhimu wa kitaifa unaolenga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya bila ubaguzi.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu wakati akizindua Rasmi Mpango wa Bima ya afya kwa wote ngazi ya Wilaya kwenye viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu Wilayani humo Februari 27,2026
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Masindi amesema kuwa jumla ya Wananchi 11,535 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo katika wilaya ya Kishapu, sawa na wastani wa Kaya 2,257 na mchango wa shilingi 150,000 kwa kila kaya kwa mwaka.
Mhe. Masindi amesisitiza kuwa mpango huo ni utekelezaji wa maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, ambaye analenga kuleta usawa katika upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote, wenye uwezo na wasio na uwezo.
“Dhamira ya Serikali ni kuona kila mwananchi anapata matibabu bora bila kujali hali yake ya kipato. Ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameleta mpango wa Bima ya Afya kwa watu wote ili kuhakikisha usawa na haki katika sekta ya afya,” amesema Mhe. Masindi.
Aidha, amewataka viongozi wa Kata, Vijiji na mitaa kushirikiana kwa karibu na wananchi katika kuhakikisha wanajitokeza kujiunga na mpango huo, huku akisisitiza kuwa afya ni msingi wa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamepongeza juhudi za Serikali kwa kuanzisha mpango huo, wakieleza kuwa utasaidia kupunguza gharama za matibabu na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kuanzia Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Mkoa hadi Hospitali za Rufaa nchi Tanzania.
Uzinduzi huo unaashiria hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya afya Wilayani Kishapu na kuendelea kutekeleza adhima ya Serikali ya kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote kwa usawa.Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akizindua Rasmi Mpango wa Bima ya afya kwa wote ngazi ya Wilaya kwenye viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu Wilayani humo Februari 27,2026 Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga Isaac Katenda akizungumza kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akizindua Rasmi Mpango wa Bima ya afya kwa wote ngazi ya Wilaya kwenye viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu Wilayani humo Februari 27,2026 Mratibu wa Bima ya Afya kwa wote Mkoa wa Shinyanga Moses Mwita akizungumza kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akizindua Rasmi Mpango wa Bima ya afya kwa wote ngazi ya Wilaya kwenye viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu Wilayani humo Februari 27,2026 Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Swalala akizungumza kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu wakati akizindua Rasmi Mpango wa Bima ya afya kwa wote ngazi ya Wilaya kwenye viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Kata ya Kishapu Wilayani humo Februari 27,2026
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin