Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MITI 1,500 YAPANDWA KISHAPU KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MHE. SAMIA ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA


Na Sumai Salum – Kishapu

Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepanda jumla ya miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye kauli mbiu isemayo "Uzalendo ni kutunza mazingira, shiriki kupanda miti".

Akizungumza kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Fatma H. Mohamed, amesema upandaji wa miti ni suala la msingi katika kulinda mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinaishi katika mazingira salama na endelevu.

Fatma amebainisha kuwa maadhimisho hayo yamebeba ujumbe mahsusi wa kuenzi maono ya Rais Samia ya kulinda mazingira na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika upandaji na utunzaji wa miti, akisisitiza kuwa kupanda mti mmoja ni kuwekeza maisha ya baadaye.
Katibu Tawala Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye zoezi a upandaji miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 27,2026

Kwa upande wake Mhifadhi  Misitu  wilayani humo, Tumaini Masatu amesema wakala huo umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kampeni za uhifadhi wa misitu na utoaji wa elimu ya mazingira, hususa kwa wanafunzi ili kujenga kizazi chenye uelewa na uwajibikaji wa mazingira.

Masatu amefafanua kuwa miti iliyopandwa itasaidia kuboresha mazingira ya shule, kutoa kivuli, kupata matunda, kupunguza athari za ukame pamoja na kuongeza uelewa wa wanafunzi juu ya umuhimu wa rasilimali za misitu.
Mhifadhi  Misitu  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Tumaini Masatu akizungumza kwenye zoezi a upandaji miti 1,500 katika Shule ya Msingi Isoso, Kata ya Kishapu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 27,2026

Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Isoso Gilbert Mtunguja ameushukuru uongozi wa Wilaya na TFS kwa kuchagua shule hiyo kuwa sehemu ya maadhimisho, akiahidi kuwa shule itahakikisha miti yote iliyopandwa inatunzwa ipasavyo.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa kwa zoezi la pamoja la upandaji miti likiwahusisha Wananachi,Viongozi,Wakuu wa Taasisi, Watumishi wa Halmashauri, TFS, Walimu na Wanafunzi, ikiwa ni ishara ya mshikamano na dhamira ya dhati ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda na kuhifadhi mazingira nchini yakiambatana na kauli mbiu isemayo "Uzalendo ni kulinda mazingira, shiriki kupanda miti".
Mkuu wa Shule ya Msingi Isoso iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani kishapu mkoani Shinyanga, Mwl. Gilbert Mtunguja akizungumza








































































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com