Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

News Alert: HAYA HAPA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2025

 


Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2025, uliofanyika kuanzia Novemba 17, 2025.

 Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 31, 2026, na Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohammed, jijini Dar es Salaam.

Jumla ya watahiniwa 569,883 kutoka shule 5,864 pamoja na watahiniwa wa kujitegemea 25,927 walifanya mtihani huo, huku mahudhurio yakifikia asilimia 97.5. 

NECTA imeeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.61 na kufikia asilimia 94.98, ambapo watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza hadi la nne.

Aidha, watahiniwa 255,404 sawa na asilimia 46.1 wamepata daraja la kwanza hadi la tatu, hali inayoonesha kuimarika kwa ubora wa elimu ya sekondari nchini.




📢 📚USAJILI WA WANAFUNZI UNAENDELEA SHULE ZA LITTLE TREASURES - 2026

Little Treasures Secondary School inawatangazia wazazi na walezi kuwa uandikishaji unaendelea kwa wanafunzi:

🎓 Wanaohamia Kidato cha Kwanza hadi cha Tatu

Vilevile, Little Treasures Pre & Primary School inapokea wanafunzi wa:

🧒 Masomo ya Awali (Pre-Primary)
📚 Darasa la Kwanza hadi la Sita

🏫 Tunatoa elimu bora yenye misingi imara ya nidhamu, maadili na ubunifu, kwa maandalizi ya kizazi chenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya duniani.

⏳ Wahi kujiandikisha sasa!

📲 Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi:

0767 211 531
0622 604 433
0745 602 164
0743 932 543

🌍 Little Treasures Schools
Prepare to Change the World

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com