Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa amesisitiza kuwa Vyombo vya Ulinzi na usalama, wakati wote vipo tayari muda wote kuhakikisha kuwa Mipaka ya nchi, Watanzania na mali zao wanabakia salama muda wote.
"Sisi kama Nchi, Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kama vilivyokuwa jana, kama vilivyo leo ndivyo vitakavyokuwa tarehe tisa Disemba na tarehe zitakazofuata.
Wakati wote Vyombo vyetu vipo tayari kuhakikisha watu na mali zao wapo salama na mipaka yetu inabakia salama. Vipo tayari si tarehe tisa tu ni wakati wote kuhakikisha nchi inakuwa salama." Amesema Msigwa.
Akizungumza na chombo kimoja cha Habari Mkoani Dar Es Salaam, Msemaji huyo wa serikali ametoa wito pia kwa Watanzania kushiriki katika kuilinda nchi yao kwa wivu mkubwa, akiwataka kutohakikisha hakuna anayeweza kuwapangia la kufanya na badala yake wafanye mambo kwa namna ya mahitaji yao wenyewe.
Msigwa kadhalika amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita ipo tayari muda wote kuwasikiliza Watanzania na kuyafanya yale yote watakayoona yanafaa kulingana na rasilimali zilizopo nchini.

Social Plugin