Na Sifa Lubasi, Dodoma
VIJANA wametakiwa kufuata hatua zinazotakiwa katika ukuaji biashara pasipo kuwa na matamanio na mafanikio ya haraka.
Akizungumza wakatii wa mahojiamo jana, Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Dodoma Crispin Kapinga alisema kuwa biashara kabla hazijaanza zina kanuni na taratibu za kufuata ili ziwe endelevu.
Amesema kuwa biashara nyingi hasa za vijana hazifanyiwi tathimini za kutosha juu ya hali halisi, masoko, kutunza mahesabu na hivyo kukosa uendelevu
"Miradi mingi ya vijana inayoendelea ni wale waliokubali kufuata hatua zinazotakiwa za ukuaji biashara pasipo kuwa na matamanio na mafanikio ya haraka, biashara ni kama mtoto haikui tu," amesema
Amesema kuwa biashara ina hatua ya kuzaliwa na wazo la unataka kufanya nini.
"Unatakiwa kuanza na wazo, kulitekeleza, hatua ya kukua ni muhimu kwani hapo wateja wanaongezeka,kila kitu kinaongezeka,pia unapofanya biashara unajifunza tabia za binadamu,"amesema
Amesema kuwa hatua muhimu ni kufanyia tathimini biashara kabla ya kuanza lakini changamoto kubwa wengi wanaanzisha biashara na kusema watajifunza mbele ya safari.
"Biashara yoyote inalenga kundi fulani. Usitangaze tu mtandaoni kuwa bidhaa inapendwa,Je inapendwa kwa kiwango gani lazima ifanyike tathimini ya kutosha na ufahamu walioko sokoni ni akina nani," amesema
Aidha amesema kumekuwa na swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini biashara nyingi zinakufa.
"Kwenye biashara lazima kuwe na wateja wenye uwezo wa kununua hizo bidhaa,, kundi la wateja." amesema
"Hakuna biashara mpya lazima ufanye tathimini ya kufahamu zile zilizo sokoni zina mipango gani,ni nani anakuwa na soko kubwa," amesema
Alisema kuwa vijana wengi wana makundi ya wateja wa mdomoni si halisia na hawana chaguo la pili hali inayopelekea biashara kukosa faida na hatimaye kufa.
Pia alisema unapomuuliza kijana uhalisia wa mtaji wengi huwa hawana majibu,wanakata tamaa
Kapinga alisema kuwa SIDO imekuwa ikishughulika na biashara ndogo ndogo,viwanda vidogo na vya kati ni vyema vijana wakawa wadadisi na kufuatilia fursa zilizopo kwenye taasisi mbalimbali.
"Fursa kama maembe mabichi,kipindi unasubiri yaive sisi tunapopoa tunakula na chumvi, kumbuka kwamba maisha yako yako mikononi mwako," alisema
Alisema kuwa vijana wengine wamekuwa wakikatisha tamaa wenzao ili wakose wote.
"SIDO inatoa ushauri wa kibiashara,kiufundi bure, ushauri wa kifedha wa namna ya kutumia na kutunza fedha, Pia kuwaunganisha na Taasisi za kifedha na Taasisi mbalimbali bila gharama yoyote.," alisema
Pia alisema SIDO wamekuwa wakishighulika na kutoa malezi na kutenga uelewa.
"Vijana wanatakiwa kutumia fursa zilizopo wajasiriamali wengi wanahitaji watu wa masoko na 'branding ',wengi wanahitaji kutangaza bidhaa kutumia mitandao ya kijamii,taarifa za fursa hawazitafuti,mwisho wa siku wao ndio wanalalamika," alisema
Aliwataka vijana kubadilika kwani kwani maisha yao yako mikononi mwao.
" Serikali kazi yake ni kutengeneza' mazingira rafiki jinsi ya vijana kufanya biashara,wakiulizwa mikopo ya Halmashuri kwa nini wanaogopa kwenda wanasema imekuwa lkitolewa kwa udugu tu je uliwahi kuomba au jus unasikia tu maneno,? alihoji.

Social Plugin