Mstahiki Meya Acton Lwankomezi akizungumza
Mstahiki Meya Acton Lwankomezi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kagondo akiapa
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mh. Acton Jasson Lwankomezi amewataka wakuu wa idara kusimamia vizuri na kutoa huduma stahiki kwa wananchi katika idara zao.
Akizungumza baada ya kiapo na uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Bukoba uliofanyika leo Desemba 2,2025 katika ukumbi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mh. Acton Jasson Lwankomezi amemtaka kila mkuu wa idara katika sehemu yake ya kazi anatakiwa kuwajibika.
Lwankomezi amesema wananchi wanahitaji kupata maendeleo na hivyo miradi yote katika maeneo mbalimbali kusimamiwa vyema na wakuu wa idara husika ili kuchochea maendeleo ya wanannchi na taifa kwa ujumla.
Viapo vya madiwani vimeambatana pamoja na uchaguzi wa Meya na naibu Meya uliofanyika leo katika ukumbi wa mkutano wa Manispaa ya Bukoba ambapo Mh. Acton Lwankomezi ameshinda kwa kura zote 20 za ndiyo pamoja na naibu Meya Mwajabu Galiatano kwa kura zote 20 za ndiyo.



Social Plugin