Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA IMESIMAMA: DUNIA YADUWAA, MAADUI WAFEDHEHEKA NA AMANI YA WATANZANIA!

Tarehe 25 Desemba, 2025, itabaki kwenye kumbukumbu za kihistoria kama siku ambayo Watanzania walionyesha ukomavu wa hali ya juu na kuiziba mdomo dunia. Wakati vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN, BBC, na majirani zetu vikiwa vimetega darubini zao vikitabiri vurugu, Watanzania wamejibu kwa Amani, Upendo, na Utulivu wa kipekee.

Kulikuwa na kampeni kubwa ya uzushi iliyopikwa na watu wasioitakia mema Tanzania. Walitamani kuona hata mtaa mmoja unawaka moto ili wapate picha za kuichafua nchi yetu mbele ya jumuiya ya kimataifa. Lakini, kwa neema ya Mungu na busara ya watoto wa Nyerere, mipango hiyo imegonga mwamba.

Kuanzia alfajiri ya Krismasi hadi leo, hakuna damu iliyomwagika, hakuna duka lililoporwa, wala hakuna sintofahamu iliyoripotiwa. Badala yake, makanisa na maeneo ya starehe yalifurika furaha, huku Watanzania wakisherehekea kwa umoja.

Baada ya kuona Watanzania wamekataa kuwa "makaa ya moto," wachochezi kama Mange Kimambi na washirika wake wameibuka na kauli za hatari na za kukata tamaa. Kwa mara ya kwanza, adui amejionyesha wazi kwa kuomba nchi yenye nguvu kama Marekani iivamie Tanzania kijeshi.

Hapa ndipo kila mzalendo anapaswa kujiuliza: Hawa watu wanaitakia nini nchi yetu?Mzalendo haombi nchi yake ipigwe mabomu;Mzalendo haombi damu ya ndugu zake imwagike;Mzalendo haombi uchumi wa nchi yake ubomolewe na kwa kuangalia kwa umakini huu unaotangazwa siyo ushindani wa kisiasa tena; huu ni uhaini na uadui wa wazi dhidi ya Taifa.

Tanzania siyo nchi ya majaribio ya vurugu. Sisi ni kisiwa cha amani na tutabaki kuwa hivyo. Wale wanaosubiri ripoti za machafuko wataendelea kusubiri hadi vidole vyao vichoke, maana Watanzania wamechagua Maendeleo mbele, Amani daima.

"Amani yetu ni tunu, na hakuna chombo cha habari wala mwanaharakati wa mtandaoni atakayeiweza nguvu ya umoja wa Watanzania."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com