Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KITUMBO ACHAGULIWA MEYA MANISPAA YA SHINYANGA, TAZAMA AKIONGOZA KIKAO CHA KWANZA BARAZA LA WADIWANI


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga ,Salum Kitumbo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mazingira ya kisiasa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yamepata sura mpya baada ya Baraza la Madiwani kumchagua Diwani wa Kata ya Mjini, Salum Kitumbo, kuwa Meya mpya wa Manispaa, huku Diwani wa Ndembezi, Pendo Sawa, akitangazwa Naibu Meya.


Uchaguzi huo, uliofanyika leo Desemba 4, 2025, umeonyesha umoja na mshikamano wa kisiasa baada ya wagombea wote wawili kuibuka na ushindi wa kura 23 za ndiyo, sawa na asilimia 100 ya wajumbe waliohudhuria.

Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, ameusimamia mchakato huo kwa mujibu wa sheria, na kutangaza matokeo hayo kwa kauli iliyoacha wazi msimamo wa baraza hilo katika kujenga kasi mpya ya maendeleo.

“Kwa mamlaka niliyopewa, natamka rasmi kwamba Salum Kitumbo ndiye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga na Pendo Sawa kuwa Naibu Meya,” amesema Kitinga mara baada ya kuhesabu kura.

Kitumbo, ambaye amekuwa akitambulika kutokana na msimamo wake mkali kwenye hoja za maendeleo na uwajibikaji, sasa anakabidhiwa jukumu la kusimamia dira ya Manispaa katika kipindi ambacho wananchi wanahitaji matokeo ya harakahasa katika miundombinu, usafi, na uchumi wa mtaa.
Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga , Pendo Sawa

Kwa upande mwingine, ushindi wa Pendo Sawa kuwa Naibu Meya unachukuliwa kama hatua ya kuimarisha mizani ya uwakilishi ndani ya baraza, ikitarajiwa kuongeza kasi ya uwajibikaji, usimamizi wa fedha za umma na kuimarisha mahusiano kati ya halmashauri na wananchi.

Mara baada ya uchaguzi huo, Baraza la Madiwani liliendelea kuunda kamati za kudumu zinazotarajiwa kusimamia miradi na sera za maendeleo, hatua inayoashiria kuanza kwa awamu mpya ya utekelezaji wa mikakati ya manispaa.

Awali, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga walikula kiapo cha udiwani kufuatia ushindi wao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mhe. Jackline Isaro akila kiapo kuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo

Zoezi hilo la uapisho, lililofanyika leo Desemba 4, 2025 katika Ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga, limeendeshwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Chibe, Mh. Agness Mlimbi, ambaye amesisitiza uzingatiaji wa sheria, maadili ya uongozi na uwajibikaji kwa wananchi.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga ,Salum Kitumbo akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani























































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com