Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA CHINA COMMUNICATIONS CONSTRUCTION COMPANY (CCCC) YAUNGANA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM(UDSM) KATIKA KUKUZA LUGHA YA KICHINA NCHINI


 Na Hellen Kwavava 

Mkurugenzi wa Utafiti na Machapisho wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dkt Mathew Senga amesema chuo hicho  kimekuwa kikiunganisha maarifa na maendeleo ya taifa toka Zamani ili kukuza lugha Mbalimbali hasa Kichina.

Dkt Senga amesema Uunganishi huo umeanza tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho  mwaka 1961.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo katika Hafla ya Uchangishaji wa Vitabu katika shubaka la Machapisho ya Kichina chuoni hapo wakati akimuwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho (UDSM)Profesa William Anangisye.

Ameendelea kusema Tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Confucius kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal mwaka 2013, kwa pamoja wamefundisha karibia wanafunzi 60,000 lugha ya Kichina.

"Shubaka la Machapisho ya Kichina  itafungua dirisha jipya kwa wanafunzi wa Dar es Salaam ili kuielewa China. Hapa, mnaweza kuchunguza siri za maendeleo ya China kupitia vitabu, mkikusanya maarifa kwa ajili ya ushiriki wa baadaye katika ushirikiano wa China–Tanzania," amesema.

Kwa Upande mwingine Naibu Meneja Mkuu, Kampuni ya China Communications Construction Company (CCCC) – Tawi la Tanzania, Deng Honglong amesema wameshiriki hafla hiyo ikiwa ni ya tatu iliyoandaliwa kwa pamoja na CCCC Tawi la Tanzania pamoja na Taasisi ya Confucius.

Honglong amesema tangu kuanzishwa kwake, mpango huo, kwa miaka mitatu mfululizo umechangia kutoa vitabu vya lugha ya Kichina na Kiingereza kwa UDSM.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi maktaba kuu UDSM, Collin Kimaryo amesema Ushirikiano huo umeimarisha rasilimali za kitaaluma na kuboresha ushirikiano wa kitamaduni kati ya Tanzania na China.

Takribani vitabu 300 vimetolewa, vikihusisha fani mbalimbali kama fasihi, sanaa na utamaduni, menejimenti, tiba, teknolojia, uhandisi na usanifu, kwa lugha za Kichina na Kiingereza.

Vitabu vitawanufaisha wanafunzi zaidi ya 20,000 na wahadhiri, kusaidia masomo, utafiti na maendeleo ya taifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com