Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

12,000 KUANZA USAHILI WA AJIRA LEO DISEMBA 13



Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuhakikisha kuwa nafasi za Ajira katika utumishi wa umma zinakuwa za wazi na za ushindani kama sera za nchi zinavyowaelekeza kupitia mchakato wa sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam, akisema tayari mpaka sasa ajira 12, 000 zimeshatangazwa na usahili wake unaanza leo Disemba 13, 2025.

"Usahili huu utafanyika kwenye Mikoa yote mtu wa Kigoma hana ulazima wa kusafiri kwenda Dodoma au Dar Es Salaam." Amesema Mhe. Waziri

Katika hatua nyingine Ridhiwani amesema ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha usahili unafanyika kwa wakati, usahili wa mchujo wa usahili huo utafanyika kielektroniki kwenye Vituo mbalimbali ikiwemo Taasisi za elimu ya juu, Vyuo vya VETA na shule za sekondari zenye maabara za Kompyuta zinazopatikana kwenye Mikoa yote na shule mahususi huko Visiwani Zanzibar.

Waziri Ridhiwani Kikwete amesisitiza pia umuhimu wa kwenda na vyeti halisi vya elimu kwa wote walioitwa kwenye usahili huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com