
***
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Kagera ambaye pia ni mkurugenzi wa chuo cha madreva cha lake zone driving school Bw. Winston Kabantega amewataka madereva wanaotaka kujifunza kuendesha vyombo vya moto kwenda katika vyuo vilivyosajiliwa na serikali.
Akizungumza na mwandishi wetu mapema leo Novemba 30,2025 katika ofisi za Radio Vision Fm Manispaa ya Bukoba Bw. Kabantega amesema kuwa, kwa miaka ya zamani ilikuwa unafundishwa na ndugu au jamaa anayejua kuendesha chombo cha moto kisha anaenda polisi kujaribiwa ambapo kwa sasa sivyo ilivyo badala yake mtu anayetaka kujifunza anapaswa kwenda katika chuo kilicho sajiliwa na serikali.
"Na mafunzo hayo kwa mujibu wa taratibu zilivyo na kipindi ambacho kimeonekana angalau huyo mshiriki wa mafunzo hapaswi kuwa chini ya wiki nne za mafunzo anayopaswa kuyapata ya msingi kitu ambacho kinaenda sambamba kwa mtu huyuhyu anayetaka kujifunza gari au pikipiki kuwa na leseni ya awali anayeipata dereva ambaye hajapata leseni"
"Leseni hiyo ni ya kipindi cha miezi mitatu ambayo inamaanisha ndani ya miezi hiyo inawezekana akawa amshaiva, lakini pia sheria imewekwa wazi kuwa vehicle inspector anaweza kumjaribu huyu aliyejifunza mafunzo ya dereva kwa kipindi cha wiki nne na kuendelea", amesema Bw. Kabantega.
Bw. Kabantega ameongeza kuwa katika kujifunza sio kukaa kwenye gari na kuendesha bali kuna mada zakujifunza ili kuelewa ikiwa nipamoja na sheria za usalama barabarani, alama za barabarani, masuala ya huduma ya kwanza, mambo ya moto na mengine mengi.
Aidha amesema kuwa, kwa utaratbu uliotolewa kuanzia tarehe 23 Septemba kwamba chuo hakitakiwi kutoa cheti kwa mwanafunzi mpaka apewe mtihani wa nadharia na vitendo kutoka jeshi la polisi na aweze kufudhu kisha awe na cheti cha macho kutoka hospital ya serikali ndipo aende TRA ili aweze kupata control namba ya kulipia leseni kamili ambayo inadumu kwa miaka mitano.
Social Plugin