Na Regina Ndumbaro, Songea – Ruvuma
Mgombea udiwani wa Kata ya Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Ngalimanayo, ameongoza maandamano ya amani yaliyosindikizwa na ngoma za asili wakati wa kurejesha fomu ya uteuzi.
Wananchi walijitokeza kwa wingi, wakiwa wamevalia mavazi ya kijani na njano, kuonyesha mshikamano na matumaini kwa mgombea wao.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Ngalimanayo alisema hatua hiyo ni mwanzo wa safari ya kuwatumikia wananchi kwa dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo.
Aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliompa tangu mwanzo wa mchakato huo na kusema kuwa umoja wao ni chachu ya ushindi katika uchaguzi ujao.





Social Plugin