Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGOMBEA URAIS SAU ACHUKUA FOMU,AWAAHIDI WATANZANIA AJIRA MILIONI KUMI




Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara, amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo akiwa na makamo wake wa Rais,Satia Mussa Bebwa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Tume huru ya Uchaguzi(INEC)leo Agosti 13 ,2025 Jijini hapa, Kyara amesisitiza kuwa kipaumbele chake cha kwanza ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini, kupunguza gharama za umeme na kuleta teknolojia za kisasa za kupikia zinazotumia nishati rafiki kwa mazingira.

Akiwa ni Mgombea wa 13 kuchukua fomu hiyo tangu mchakato huo utangazwe na INEC,Kyara amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuwatumikia,Serikali yake itashirikiana na kampuni zinazotengeneza majiko ya nishati safi ili kuhakikisha wananchi, hususan wale walioko pembezoni, wanapata nishati safi na nafuu.

Mbali na hilo, Kyara ameeleza azma yake ya mapinduzi ya kiuchumi katika sekta za viwanda, kilimo na teknolojia, akiahidi kuunda ajira milioni 10 kwa vijana ndani ya miaka mitano.

“Tunataka kumkomboa Mtanzania, kutoa fursa za ajira na kuhakikisha maendeleo yanagusa kila kaya,” amesema.

Mgombea huyo ametangaza sera za kupambana na ajira zisizofaa kwa watoto wa kiume, kuhakikisha bei za mafuta kwa wananchi wa pembezoni ziwe nafuu, na kurekebisha maslahi ya walimu ikiwa ni pamoja na mishahara ya wakati na mazingira bora ya kufundishia.

Kyara amesisitiza pia kurejesha mchakato wa katiba mpya, akisema: “Tunakwendza kuzindua katiba mpya ndani ya siku 40 baada ya kuunda serikali yenye uwazi, haki na maendeleo endelevu.”

Kwa sasa, baada ya kuchukua fomu, Kyara na timu yake wanakusanya wadhamini na sauti ya umma ili kuanza rasmi kampeni, ambapo mgombea huyo amesema hatua hiyo muhimu itaenda sambamba na kujenga taifa lenye hofu ya Mungu, likiwa na utaratibu thabiti wa maendeleo, haki yanayolenga kuondoa umasikini na kukuza ajira kwa vijana.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com