Na Mwandishi Wetu Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, amewataka Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli na programu mbalimbali zinazoratibiwa na Ofisi hiyo ili kuongeza uelewa wa umma.
Bi. Meena alitoa wito huo leo, Agosti 2, 2025, alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma, akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Stephen Nindi, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri.
“Wananchi wana uhitaji mkubwa wa kufahamu shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni muhimu kuwa na vipindi na kampeni endelevu za kuelimisha umma ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinawafikia walengwa,” amesema Bi. Meena.
Maonesho ya Wakulima ya Nanenane kwa mwaka huu yanafanyika yakibeba kaulimbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”



Social Plugin