Na Woinde Shizza ,Arusha
Katika kuunga mkono jitihada za wakulima wa Tanzania na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, benki ya CRDB wamekuja na Mradi wa TACATDP (Tanzania Agricultural Catalytic Trust Development Program) ambao utawasaidia wakulima kwa vitendo kupitia mikopo nafuu, teknolojia rafiki na elimu ya kifedha.
Wakiwa katika Maonesho ya 31 ya Kilimo (Nane Nane) yanayoendelea Themi Njiro mkoani Arusha, wameweka banda lao wazi kwa wananchi wote kujifunza na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa kilimo na fedha.
Akiongea na waandishi wa habari Hamid Mwakombe, Meneja wa Mahusiano wa TACATDP Kanda ya Kaskazini, lengo lao kuu ni kuhakikisha wakulima wote wakiwemo vijana na wanawake wanapata fursa ya kufanya kilimo cha kisasa, chenye tija na endelevu.
“Tunatoa mashine zinazotumia nishati ya jua (sola) kwa ajili ya kusukuma maji shambani, mbolea asilia inayolinda ardhi, pamoja na mikopo ya ujenzi wa vitalu vya kilimo ,Haya yote ni kwa ajili ya kumuinua mkulima mdogo aweze kulima bila wasiwasi wa mabadiliko ya tabianchi,” alisema Mwakombe.
Aidha, aliwahimiza wananchi wote, hasa wakazi wa mikoa ya kaskazini, kufika kwenye banda lao ndani ya viwanja vya Nane Nane ili wapate elimu ya kilimo bora, namna ya kufungua akaunti, jinsi ya kuandika maandiko ya kilimo, na kuelewa vigezo vya kupata mkopo wa kilimo kutoka CRDB.
“Hatuishii kwenye kutoa mikopo tu, bali tunatembea na mkulima bega kwa bega kwani tunataka wakulima wetu walime kwa maarifa, watumie teknolojia sahihi na waweze kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo,” aliongeza.
Alibainisha kuwa Mpango huu wa TACATDP unaendelea kuwa tumaini jipya kwa wakulima wote wanaotamani kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia kwenye kilimo biashara Kwa ambapo wakulima wanapewa kila nyenzo muhimu ya kuwasaidia kufikia mafanikio.
Aidha aliwasihi wananchi kutembelea banda la CRDB lililopo katika maonesho ya Nane Nane Themi Njiro, ili kujifunza zaidi, kuuliza maswali, na kupata huduma moja kwa moja kutoka kwa wataalamu waliopo.



Social Plugin