
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi majina ya wagombea wake wa ubunge watakaowania katika majimbo saba ya Mkoa wa Shinyanga katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Katika uteuzi huo, majina ya waliopitishwa ni kama ifuatavyo:
Benjamin Lukubha Ngayiwa – Jimbo la Kahama Mjini
Mabula J. Magangila – Jimbo la Msalala
Ahmed Salum – Jimbo la Solwa
Azza Hillal Hamad – Jimbo jipya la Itwangi
Emmanuel Cherehani – Jimbo la Ushetu
Patrobas Katambi – Jimbo la Shinyanga Mjini
Lucy Mayenga – Jimbo la Kishapu
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, wagombea hao wamepitishwa baada ya mchakato wa kura za maoni na kupitia vikao vya juu vya uteuzi wa CCM, hatua inayohitimisha safari ya ndani ya chama kuelekea katika kinyang’anyiro cha ubunge mwaka huu.
Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa ngome muhimu za kisiasa nchini ambapo CCM imekuwa ikifanya vizuri katika chaguzi zilizopita. Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umuhimu wa majimbo ya eneo hilo kiuchumi na kijamii, hasa kutokana na shughuli za kilimo, biashara na uchimbaji madini.
Wananchi sasa wanasubiri kuona sera na ahadi za wagombea hao katika kampeni rasmi zinazotarajiwa kuanza baada ya uteuzi wa INEC.
Social Plugin