Na Mwandishi wetu - KAHAMAUchaguzi wa Madiwani wa Viti maalum katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Umoja wa Wanawake (UWT) katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umetamatika ambapo jumla ya washindi 23 wamepatikana kati ya watia nia 90 waliomba kuchaguliwa.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo Erenestina Richard ambaye ni Katibu CCM wilaya ya Shinyanga vijijini amesema washindi hao wanatoka katika tarafa sita zinazounda wilaya ya Kahama ambapo katika tarafa ya Kahama Mjini Thelesiphora Saria amepata kura 1093,Eritha Makaga kura 954,Rehema Joshua 948 na Merry Charles kura 314.
Katika tarafa ya Isagehe walioshinda ni pamoja na Scholastica Shija kura 840,Mpaji Mwalimu kura 839 na Winifrida Petre kura 462 huku katika tarafa ya Msalala ni Mariamu Mkwiwa 933, Nyagwema Warioba kura 650,Hamisa Kalinga kura 567 na Grace Masanja kura 547.
Amesema washindi wengine wanatoka katika tarafa ya Isagehe Msalala ambao ni Pili Izengo kura 499,Mwashi Madata kura 501,Matha Shedrack kura 478 huku katika tarafa ya Dakama walioshinda ni Betha Leornad kura 733,Yulitha Msafiri kura 765,Festa Kabasa kura 767,Eva Pius kura 514 na Maria Maziku kura 471.
Washindi wengine wanatoka katika tarafa ya Mweli ambao ni Asha Marco kura 1053,Esta Matone kura 1042 ,Helen John kura 612 huku mkutano huo ukiwa na Wajumbe 3807.
Social Plugin