
Katika uamuzi huo uliotolewa mbele ya jopo la Majaji watatu - Jaji Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dkt. Benhajj Masoud - Mahakama ya Rufani ilipitia hoja mbalimbali ikiwemo:
Iwapo Mahakama Kuu ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, Iwapo mdai (Mchechu) aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa, Iwapo Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu na fidia.
Majaji walikubaliana na hoja za wakili wa upande wa Nehemia Mchechu, Wakili Aliko Harry Mwamanenge, na kueleza kwamba Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo, na kwamba mdai aliwasilisha ushahidi thabiti kuthibitisha kuwa alidhalilishwa. Pia, Mahakama Kuu ilifuata misingi sahihi ya kisheria katika kutoa nafuu na fidia.

Social Plugin