JAMAA ABAKA KUKU HADI KUFA KWENYE KOCHI MWANZA...AKAMATWA AKISEMA NI 'HAMU TU'


Katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sunday mkazi wa kitongoji cha Misungwi kata ya Usagara wilaya Misungwi  Jijini Mwanza anatuhumiwa kubaka kuku hadi kufa.


Wakizungumza na EATV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa alimkamata kuku huyo ambaye alikuwa anataga kisha kumuingiza ndani ya nyumba yake na kuanza kumbaka na baada ya kumaliza haja zake alienda kumtupa nje.

Delifina Boazi ni mmoja wa wapangaji katika nyumba hiyo amesema alitoka nje kwenda kukinga maji bombani ndipo alipomuona mtuhumiwa akifanya kitendo hicho sebleni akiwa amekaa kwenye makochi


"Nilimuoma alikuwa amemkamata kuku na anafanya naye mapenzi na alipomaliza alienda kumtupa," amesema Delifina.


Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa kitongoji cha Misungwi, Samson Madirisha amekiri kupokea taarifa hizo na baada ya kufika eneo la tukio alikuta kitendo hicho kufanyika.

Madirisha amesema baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa alikuwa na hamu hivyo alishindwa kujizuia.

Naye Kamanda wa Sungusungu kata ya Usagara, Buhili Makubilo na mkazi wa eneo hilo Edista Mganga wameviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wanaobainika kufanya vitendo hivyo.

Hata hivyo polisi wilaya ya Misungwi wamefika kwenye nyumba ya mtuhumiwa na kumchukua kwa ajili ya mahojiano zaidi. Chanzo EastAfricaTV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم