SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA AL AHLY, YACHAPWA 1-0


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kukubali kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.

Katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza Al Ahly walifanikiwa kupata bao la Mapema kupitia kwa Ahmed Kouka dakika ya 4 ya mchezo kipindi cha kwanza.

Timu hizo zitarudiana Aprili 5, 2024 ambapo Al Ahly kwenye mchezo huo atakuwa nyumbani mjini Cairo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم