NCHI 140 KUSHIRIKI MICHEZO YA CISM DAR


Na Dotto Kwilasa,DODOMA

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Francis Mbindi ameeleza kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM),litakalo husisha nchi wanachama 140 kutoka mabara yote Duniani.

Aidha katika mkutano huo Ujio wa wageni utakuwa na fursa kwani nchi na jeshi litajulikana kupitia maeneo mbalimbali kiuchumi, kisiasa na kijamii na kutangaza lugha ya Kiswahili .

Mwenyekiti hiyo ameeleza hayo jana jijini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano huo ambapo amesema nchi wanachama 140 kushiriki mkutano huo huku akieleza kuwa jumla ya lugha tano zitatumika zikiwemo Lugha ya Kingereza, Kispania, kifaransa kiarabu na kiswahili chenyewe.

Aidha amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi duniani ambapo jumla ya wageni 300 kutoka nchi .

Amesema Baraza hilo lilianzishwa mwaka 1945 linaumuhihgimu mkubwa kwani lengo ni kukutanisha shughuli za Michezo na utimamu wa kimwili badala ya kutumia vita.

" Dhima ni Nchi wanachama kukutana katika viwanja vya Michezo kuimarisha ushirikiano badala ya kukutana kwenye viwanja vya vita,"amesema .

Amesema mkutano huo wa siku saba ambapo utaanza rasmi tarehe 12 Mei hadi 19 Mei 2024 ambapo washiriki wa mkutano huo watatembelea vivitio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

" Kwakuwa Mkutano huu ni wa kijeshi basi maeneo yote yaliotoa mchango wa nchi kupata Uhuru yatatembelewa ukiwemo Mnara wa mashujaa uliopo Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam,"amesema

Aidha amesema mwaka 1991 Tanzania iliwahi kuwa mwenyeji na mkutano ulifanyika Jijini Arusha ambapo washiriki waliweza kutembelea Mbuga za wanyama zilizopo Jijini Arusha.

" Matarajio yetu ujio wa wageni wetu utakuwa wa manufaa makubwa kama ilivyokuwa 1991 , " Amesema

Hata hivyo katika Mkutano huo kauli mbiu unasema " Urafiki Kupitia Michezo na utafungwa tarehe 17 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Michezo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Kanali Martin Msumari amesema kuwa kutakuwa na michezo ya kipaumbele ambayo ni pamoja na riadha, vile vile mchezo wa ngumi na michezo mbalimbali itakuwepo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments