KAMATI YA UTEKELEZAJI JUMUIYA WAZAZI CCM TAIFA KUTINGA KAGERA


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Kagera Hamimu Mahmudu

Na Mariam Kagenda - Kagera
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya wazazi CCM Taifa inayoongozwa na mwenyekiti Fadhir Rajab Maganya ambaye ni mjumbe wa kamati kuu wanatarajia kufanya ziara ya siku tano mkoani Kagera kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Akizungumza na vyombo vya habari Februal 26,2024 Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama hicho mkoa wa Kagera Hamimu Mahmudu amesema ziara hiyo inatarajiwa kuanza Machi nne mwaka huu ambapo itashirikisha mwenyekiti,makamu wake pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Taifa na baada ya kupokelewa watagawanyika makundi mawili ili kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi.


Hata hivyo Mahmudu amesema kundi moja litaongozwa na mwenyekiti ambapo watakwenda katika Wilaya za Biharamulo,Ngara,Kyerwa,Karagwe na Bukoba Manispaa na jingine kuongozwa na makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa ambapo watatembelea Wilaya za Muleba,Bukoba vijijini na Missenyi kisha wote kukutana na kufanya majumuisho Machi nane mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments