MLANDEGE FC YAINYUKA SIMBA SC 1-0, YANYAKUA KOMBE LA MAPINDUZI CUP


NA EMMANUEL MBATILO,

KLABU ya Mlandege Fc imefanikiwa kuutetea ubingwa wake mara baada ya kuichapa Simba Sc bao 1-0 kwenye fainali ya michuano ya Mapinduzi Cup ambayo ilikuwa inaendelea visiwani Zanzibar.

Katika mchezo huo ambao Simba Sc ilifanikiwa kuutawala mchezo kwenye vipindi vyote licha ya kutofanikiwa kupata bao huku wakiruhusu kufungwa bao moja na kushindwa kunyakua taji hilo.

Bao pekee ambalo limewafanya Mlandege Fc kuibuka washindi limefungwa na Joseph Akandwanao mnamo dakika ya 54 ya mchezo baada ya kuwatoka mabeki wa Simba Sc na kupiga shuti kali lililomshinda kipa na kuingia nyavuni.

Ikumbukwe Mlandege Fc kabla ya fainali haijawahi kushinda ndani ya dakika 90 kwenye michuano hiyo ya kipindi hiki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments