Tanzia : MMILIKI WA MASWA YETU BLOG INNOCENT MBWAGA MAARUFU BLOGGER BOY AFARIKI DUNIA

Innocent Mbwaga enzi za uhai wake
Mwendeshaji na Mmiliki wa Mtandao wa MASWA YETU BLOG, Innocent Lugano Mbwaga maarufu Blogger Boy amefariki dunia.

Innocent mkazi wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu ambaye ni Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara amefariki dunia  leo asubuhi Ijumaa Desemba 8,2023 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda ya Kusini - Mtwara  baada ya kupata ajali ya pikipiki Tandahimba Desemba 5,2023.

"Ni kweli kijana wangu kafariki dunia leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kanda Mtwara, alipata ajali ya pikipiki siku ya Jumanne akitokea kazini kwake Tandahimba...Taarifa zaidi tutaendelea kupeana", amesema baba mzazi wa Innocent mzee Mbwaga.

Mazishi  ya mwili wa  Innocent Mbwaga (Blogger Boy) yatafanyika siku ya Jumatatu Desemba 11, 2023 nyumbani kwao Maswa Mjini (Njia panda ya Lalago) mkoani Simiyu 


R.I. P Innocent Mbwaga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

10/Post a Comment/Comments

 1. Rest in peace

  ردحذف
 2. Daah inauma sana . Pumzika kwa amani mtaalamu wetu

  ردحذف
 3. Pigo jingine kwa tasnia ya habari na teknolojia.

  ردحذف
 4. Inaumiza sana kiukweli alikuwa jamaa yetu sana one class SUA 2016

  ردحذف
 5. nimelia sana tena sana inno rafiki yangu umeniacha. mungu akupumzishre salama . namshukuru mungu kwa kila jambo

  ردحذف
 6. pumzika salama inno rafiki yangu . namshukuru mungu

  ردحذف
 7. Pumzika kwa amani sir

  ردحذف

إرسال تعليق