ZOEZI LA MABORESHO DAFTARI LA WAPIGA KURA KUFANYIKA NG'AMBO TABORA NA IKOMA RORYA MKOANI MARA

Meza kuu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Bw. Jacob Mwambegele katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,

*****************

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uboreshaji wa majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kata ya Ng’ambo iliyopo mkoani Tabora na Ikoma iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Mkoani Mara.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 16,2023 katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Bw. Jacob Mwambegele amesema uboreshaji wa majaribio utafanyika kuanzia Novemba 24 hadi 30, 2023 na umepangwa kufanyika katika vituo 16 ambapo vituo 10 ni vya kata ya Ng’ambo na vituo sita (6) vipo kata ya Ikoma, na vilevile vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.


"Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kupima uwezo wa vifaa na mifumo ya uandikishaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe na ratiba itakayopangwa na Tume". Amesema 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima amesema kuwa uboreshaji wa majaribio utahusisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na atayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine, waliopoteza au kadi zilizoharibika, wanaorekebisha taarifa zao na kuondoa wapiga lura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari.

Amesema katika kufanikisha zoezi hilo, Tume itatumia vifaa mbalimbali vya uandikishaji yaani (BVR kits) ambazo zimeboreshwa na zina uwezo wa kuwasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura na ni tofauti na zile zilizotumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015 na 2019.

Hata hivyo amesema kuwa Tume imesanifu na kuboresha mfumo wa uandikishaji wa Wapiga Kura ili kukidhi muundo wa BVR Kits za sasa ambazo zinatumia programu ya android tofauti na BVR Kits za awali ambazo zilikuwa zinatumia programu ya Microsoft Windows.

“Mfumo wa uandikishaji ulioboreshwa utawawezesha wapiga kura ambao wameshaandikishwa na wapo kwenye daftari la wapiga kura kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zao ama kwa kubadilisha kituo cha kupigia kura iwapo amehama Mkoa au Wilaya nyingine au kurekebisha taarifa zao kwa njia ya mtandao kwa kutumia simu zao za mkononi au kompyuta,” amesisitiza Bw.Kailima.

Ameongeza kuwa kuanzisha mchakato mtandaoni mpiga kura ataingia kwenye tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni www.nec.go.tz kwa kutumia kompyuta au simu janja kisha atabonyeza kiunganishi kilichoandikwa “Boresha Taarifa za Mpiga Kura” au atatumia anuani ya ovrs.nec.go.tz itakayompeleka moja kwa moja kuanzisha mchakato.

Kailima amesema vyama vya siasa vitashiriki kwa kuweka wakala mmoja kwa kila kituo cha kuandikisha wapiga kura ili waweze kushuhudia na kujiridhisha kuhusu taratibu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa majaribio wa Daftari.

Pamoja na hayo amesema kuwa utaratibu wa kuboresha taarifa kwa njia ya mtandao, hautawahusu wapiga kura wanaotaka kuandikishwa kwa mara ya kwanza na wapiga kura ambao kadi zao zimeharibika au kupotea.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Bw. Jacob Mwambegele akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Chama Cha AAFP, Bw.Rashid Rai (kushoto) akiwa katika katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Chama Cha ADC, Bw. Doyo Hassan Doyo akiwa katika katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika akiwa katika katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Bw. Eugene Kabendera akiwa katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wakifurahi jambo wakati wa Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Bw. Jacob Mwambegele akipata picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa ucahguzi katika Mkutano wa Kitaifa wa NEC na Vyama Vya Siasa, kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uliofanyika leo Novemba 16,2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam,

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم