TAKUKURU SHINYANGA YABAINI MIL. 83.3 KODI YA ZUIO KUTOWASILISHWA TRA


TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Shinyanga, imebaini kiasi cha Tshs million 83.3 za kodi ya zuio kutowasilishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka wa wazabuni na watoa Huduma katika mkoa wa Shinyanga na Kufanya serikali kupoteza mapato.

Akisoma taarifa ya uchunguzi huo kwa vyombo vya habari mapema leo Septemba 06, 2023 katika ofisi za TAKUKURU Mkoani Shinyanga.

Kaimu mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani humo Mwamba Masanja amesema uchambuzi huo ulibaini kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya Sh. 83,328,256.81 fedha za kodi ya zuio zilizokatwa kutoka kwa wazabuni na watoa huduma hazikuwasilishwa kwa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA.

 “Tumebaini kuwa zaidi ya milioni 83 fedha za fedha za kodi ya zuio zilizokatwa kutoka kwa wazabuni na watoa huduma hazikuwasilishwa kwa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato Tanzania TRA kama sheria inavyoelekeza, sababu zilizopelekea kutowasilishwa kwa fedha hizo ni pamoja na mabadiliko ya mfumo wa TRA (Tax Payer Portal), uelewa mdogo juu ya mapato hayo pamoja na wazabuni na watoa huduma kutokudai stakabadhi za makato ya kodi ya zuio waliyokatwa”, alisema Mwamba Masanja.

Aidha Masanja amesema TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika  kipindi hicho yenye thamani ya shilingi Bilioni 16.2 na kubaini dosari ndogondogo kwenye miradi ya sekta ya elimu, afya, maji na ujenzi.

“Mradi wa ujenzi wa kituo cha afya bulige haujakamilika na ujenzi wa shule ya msingi maganzo umebainika kuwa jengo la utawala halijawekwa vigae, roof board haina ubora, vyoo vya wavulana kukukosa ventilation, madarasa ya chekechea mikanda ya gypsum boadi imeanza kubanduka na bembea upande wa chekechea hazijawekwa”, alisema Masanja.


 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments