AMUUA MUMEWE ILI AOLEWE NA MWANAUME MWINGINE


Jeshi la Polisi mkoa Morogoro limewatia mbaroni watuhumiwa wawili  Maela Athanas (33) na Holo Jilia (45) wote  wakazi wa Kilolero B kwa kosa la kumuua  Charles Maghashi (55) mkulima  mkazi wa Kilolero B . 

Tukio hilo lilitokea mnamo Oktoba 29, 2023 ambapo Maela Athanas alikwenda nyumbani kwa marehemu na kumkuta amelala sebuleni kwake na kuanza kumkata na kitu chenyewe ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo chake.

Jeshi la Polisi baada ya kufanya uchunguzi limebaini kuwa, mke wa marehemu ambaye ni Holo Jilai alikula njama ya kumuua mume wake Charles Maghashi ambapo alimtuma Maela Athanas kutekeleza mauaji hayo kwa ahadi ya kumlipa pesa shilingi laki tisa (900,000) ambapo malipo ya awali alimpatia kiasi cha  elfu hamsini (50,000)  ili aweze kutekeleza mauaji hayo.

Aidha taarifa za mwanzo zinaeleza kuwa Holo ambaye ni mke wa Marehemu alimtaka Mme wake waachane lakini Maghashi akikataa na ndipo Holo alichukuwa uamzi huo wa kumuua mme wake ili apate nafasi ya kuolewa na mwanaume mwingine.

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments