DUCE YAIPONGEZA SERIKALI KUENDELEA KUTOA RASILIMALI MUHIMU ZA UENDESHAJI CHUO

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu wakisimama kwaajili ya wimbo wa Taifa wakati Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu muhimu na kutoa fedha za uendeshaji wa Chuo Kishiriki Cha Elimu (DUCE) ambapo pia imeendelea kuongeza wigo wa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya Juu wakiwemo wanafunzi wa chuo hicho.

Ameyasema hayo leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. William Anangisye wakati wa Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo hicho.

Aidha Prof. Anangisye ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa rasilimali muhimu zinazohitajika katika uendeshaji wa Chuo hicho ambapo pia amewataka wahitimu kuendelea kuwa sehemu ya uchangiaji wa shughuli mbalimbali za chuo.

Pamoja na hayo amesema kuwa chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi ili kuhakikisha malengo ya kuanzishwa kwa chuo hicho yanafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.

"Chuo kinakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kutoendana na kasi ya kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi na gharama kubwa ya kusomesha wanataaluma". Amesema Prof. Anangisye.

Kwa upande wake Kaimu Rasi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Maluka amesema kupitia Mradi wa HEET Chuo kinatarajia kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni Kumi kwaajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu na majengo ya Chuo, kujenga majengo mawili ya ghorofa sita na miundombinu mingine mipya.

"Kwa sasa, Mkataba na mshauri Elekezi kwa ajili ya Usanifu na Usimamizi wa ujenzi umesainiwa tarehe 13 Oktoba 2023 ili kufanya kazi hiyo, na inatarajiwa kuwa kufikia Januari 2024, shughuli hizi za ujenzi zitakuwa zimepamba moto". Amesema 
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatunuku Digrii za Awali na Uzamili wahitimu wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwenye Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza wahitimu wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) waliofanya vizuri kwenye masomo yao wakati wa Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakiwa kwenye maandamano katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare akizungumza katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare akisoma hotuba yake katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. William Anangisye akisoma hotuba yake katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Rasi wa Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. Stephen Maluka akisoma hotuba yake katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Rasi-Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt. Christina Raphael akizungumza katika Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof. William Anangisye wakati wa Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwenye Mahafali ya 16 Duru ya Pili ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Novemba 28,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم