PROF. MKENDA KUTOA TUZO ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA WAANDISHI HABARI

Mshindi wa Mwaka 2023 katika mashindano ya uandishi bora wa habari za sayansi na kilimo (Bioteknolojia) katika kuendeleza Kilimo, Lucy Ngowi kutoka Gazeti la habari leo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi toka Tume ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) kushoto sambamba na Mkurugenzi mstaafu kutoka Tume hiyo upande wa kulia Dkt. Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Tume ya sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.

Na HELLEN ISDORY KWAVAVA - Dar es salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika Tuzo za Waandishi wa Habari za Sayansi na teknolojia hususani Bioteknolojia zitakazofanyika Desemba Mosi mwaka huu Jijini Dar es Salaam.


Hayo yamesemwa na Afisa mratibu wa programu za AATF Bw. Verenardo Meeme leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa sherehe za ugawaji wa Tuzo hizo zitafanyika katika Hoteli ya White wa Sands iliyoko jijini Dar es salaam.


Aidha Meeme ametumia nafasi hiyo kuwataka waandishi wa habari kujikita zaidi katika kuandika habari za sayansi kwa kuongea ukweli kupitia watafiti mbalimbali ambao wamefanya tafiti za kisayansi ili jamii ipate manufaa ya kupitia wataalamu hao.


“Ipo haja kwa wananchi pia kujua kuhusiana na Bioteknolojia ili kuondoa sintofahamu iliyojengwa kwenye vichwa vya wengi ambapo Tanzania bado iko nyuma ukilinganisha na nchi nyingine zinazofanya utafiti wa Bioteknolojia hususani nchi ya Kenya”, amesema Meeme.

Tuzo hizo ni za nane toka zimeanzwa kutolewa Jukwaa la Bioteknolojia ya Kilimo Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo Afrika(AATF) na nchi 11 za Afrika zinatarajia kushiriki ikiwemo Malawi, Rwanda, Msumbiji, Kenya, Uganda, Tanzania, Burkinafaso, Nigeria, Ghana, Ethiopia na Afrika Kusini ambapo Waaandishi washiriki katika Tuzo hizo ni kutoka katika nchi hizo isipokuwa Afrika Kusini pekee.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم