ALIYEFUFUKA AKIZIKWA AFARIKI RASMI BAADA YA SIKU TANO


Mwanamke mwenye umri wa miaka 76, kutoka Ecuado amefariki dunia wiki moja baada ya kutangazwa kufufuka siku ya maziko yake.

Katika tukio hilo lililotokea Amerika ya Kusini , Bella Montoya alishangaza jamaa zake waliokuwa wanamuomboleza kwa kugonga jeneza lake mwenyewe wakati wa ibada yake ya mazishi.

Baada ya kufungua jeneza, waombolezaji walishangazwa kuona kwamba mama huyo mzee bado yuko hai na haraka wakamrudisha hospitalini. 

Walakini, hali yake ilikuwa bado mbaya. Wiki moja baada ya kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi, Wizara ya Afya ya Ecuador ilitangaza muuguzi huyo mstaafu aliyefufuka alifariki kutokana na kiharusi.

"Wakati huu, mama yangu alikufa kweli. Maisha yangu hayatakuwa kama zamani," alisema Gilbert Barbera, mtoto wake Montoya, kama alivyonukuliwa na BBC. 

Tukio hilo la kushangaza limesababisha serikali kufanya uchunguzi kuhusu hospitali iliyohusika, likiibua maswali kuhusu taratibu za matibabu na usahihi wa vyeti vya kifo.

Kamati ya kiufundi ilibuniwa kuchunguza jinsi hospitali inavyotoa vyeti vya kifo, ilisema taarifa kutoka wizara hiyo.

Montoya alikuwa amelazwa hospitalini tarehe Ijumaa, Juni 9, 2023 kwa uwezekano wa kupatwa na kiharusi na kusimama kwa moyo na mapafu, na baada ya kushindwa kujibu jitihada za kumrejesha kwenye hali ya uhai, daktari aliye kuwajibika alitangaza kifo chake, ilisema wizara hiyo. 

Baadaye, familia ilimpeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti na ilikuwa ikifanya shughuli za mazishi wakati walipoanza kusikia sauti za ajabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم