TGNP YAWATAKA VIJANA WA KIKE KUJIKITA ZAIDI KWENYE MASUALA YA TEKNOLOJIA



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Jamii hasa kwa vijana wa kike wametakiwa kujikita katika masuala ya Sayansi, Teknolojia ya Uhandisi na Hisabati ili kuweza kuwapata wataalamu Wanawake wa kutosha wa masuala ya sayansi, Teknolojia ya Uhandisi na Hisabati na kuweza kulisaidia Taifa hapo baadae.

Wito huo umetolewa na Prof. Verdiana Masanja leo Machi 10,2023 Jijini Dar es Salaam wakati akielezea safari yake ya maisha katika kupendelea somo la Hisabati akiwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) .

Amesema katika baadhi ya mataifa yamekuwa yakishindwa kuwathamini wanawake wasomi hasa wale wataalamu wa somo la hisabati wanaotokea katika bara la Afrika kwani hilo limetokea kwa upande wake akiwa masomoni nje ya nchi.

Amesema tafiti zilifanyika na kuona sababu zinazopelekea wasichana kutopenda kujiingiza katika masuala ya teknolojia ni kutokana na kutokujiamini kwamba anaweza, kuaiminishwa mambo ya teknolojia si ya wanawake kwa sababu wanawake hawaonekani kwenye masuala hayo.

"Majumbani kwetu, chochote kinachohusiana na teknolojia kikiharibika anaitwa mvulana kuja kukirekebisha, sasa vitu kama hivi tangu akiwa mdogo dhana ile inaenda inajengeka anajua mambo hayo ni kwa ajili ya wanaume na si kwa wanawake",amesema.

Amesema Serikali imerahisha kwenye suala la elimu bila malipo, hivyo mabinti wanatakiwa kutumia fursa hiyo kufanya vizuri kwenye masomo yao na kuweza kuzalisha wasomi wanawake wengi katika taifa letu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TGNP Bi. Lilian Liundi amesema TGNP imekuwa ikifika katika maeneo ya pembezoni ambayo si rahisi kufika ili kuhakikisha jamii inapata uelewa mkubwa kuhusiana na usawa wa kijinsia.

Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo yamefanyika kwa siku mbili kati ya Machi 9- 10,2023 kwenye Viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam Profesa wa Hisabati ,Prof. Verdiana Masanja akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo yamefanyika kwa siku mbili kati ya Machi 9- 10,2023 kwenye Viwanja vya TGNP Jijini Dar es SalaamMkurugenzi wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo yamefanyika kwa siku mbili kati ya Machi 9- 10,2023 kwenye Viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo yamefanyika kwa siku mbili kati ya Machi 9- 10,2023 kwenye Viwanja vya TGNP Jijini Dar es SalaamBaadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo yamefanyika kwa siku mbili kati ya Machi 9- 10,2023 kwenye Viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments