RC DODOMA APOKEA TUZO YA RAIS SAMIA NI KATIKA MASUALA YA MAENDELEO YA  ELIMU.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akimkabidhi Tuzo ya Heshima Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule iliyotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake Katika maendeleo ya sekta ya Elimu nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule kwa kumpongeza yeye pamoja na wasaidizi wake katika kuongeza ufaulu mkoani humo iliyotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera,akielezea tuzo zilizotolewa na taasisi hiyo kwa viongozi kwa kutambua mchango wa Elimu nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule,akiipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inazofanya katika sekta ya elimu kwenye mikoa mbalimbali nchini wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu,akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa Sekta ya Elimu katika Mkoa wa Dodoma.




Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara,Hezbon Mwera ,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule ,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.


SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.



Na.Alex Sonna-DODOMA

TAASISI ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara inayojishughulisha na masuala ya elimu imempa tuzo Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule na Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hezbon Mwera Machi 30, 2023 katika mkutano wa wadau wa sekta ya elimu Mkoani Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Prof. Mwera,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo,Hezbon Mwera amesema kwa kutambua jitihada na mchango katika sekta ya elimu unaotolewa na Rais Samia wameamua kumpa tuzo hiyo ya heshima.

Amesema Taasisi hiyo inajishughulisha na mambo ya kijamii na wamepewa kibali na ofisi ya Tamisemi kufanya shughuli zao ndani ya Mikoa 10 ya Tanzania.

Amesema shughuli wanazozifanya ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vyuo vya ufundi kwani kila mmoja anajua umuhimu wa vijana kupata mafunzo ya Elimu ya ufundi baada ya kumaliza darasa la saba na kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo.

"Nipende kumpongeza Rais Samia kwa kuanzisha vyuo katika kila Wilaya.Taasisi yetu hii pia inashirikiana na Ofisi za Mikoa kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya darasa la saba, kidato Cha nne na sita,"amesema

Mkurugenzi huyo wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa, amesema wametoa tuzo katika Mikoa ya Mwanza,Kigoma,Simiyu,Shinyanga,Geita ,Mara.

Pia alimkabidhi tuzo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa kumpongeza yeye pamoja na wasaidizi wake katika kuongeza ufaulu mkoani humo.

Tuzo za jumla zilizotolewa katika hafla hiyo zilidhaminiwa na taasisi ya ya Professor Mwera Foundation ya mkoani Mara.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mh. Rosemary Senyamule,ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inazofanya katika sekta ya elimu kwenye mikoa mbalimbali nchini.



RC Senyamule amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa kuhakikisha watoto wote wanaenda shuleni na matarajio ya Serikali ya awamu ya sita ni kuona elimu bora inatolewa pamoja na changamoto zote zinatatuliwa.

"Ili Mkoa uweze kusonga mbele kielimu ni lazima tuhakikishe watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa na wanahudhuria shule wakati wote,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkuu huyo wa Mkoa ameupongeza Mkoa huo kwa kushika nafasi ya 10 kitaifa kwa matokeo ya mwaka 2022.

"Niendelee kusisitiza yale tutakayokubaliana tukayatekeleze,niwaombe tuzidi kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Naye,Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu,amesema wataliendeleza tukio hilo na litakuwa la kila mwaka.

Amesema ili ipatikane Dodoma yenye maendeleo lazima wawe wamoja katika kusimamia ubora wa elimu.

Amesema lengo la kikao hicho ni kuangalia namna bora ya kuongeza ubora wa elimu mkoani humo na kuongeza ufaulu wa Kitaifa.

Ameyataja malengo ya Mkoa ni kutoka katika asilimia 83.01 mwaka 2022 hadi 85 kwa mwaka 2023 katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Amelitaja lengo la pili ni kutoka asilimia 91.27 mwaka 2022 Hadi 100 mwaka 2023 katika upimaji wa elimu kitaifa katika darasa la nne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments