TRA SHINYANGA YATOA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WAFANYABIASHARA

Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga wakitoa elimu ya mlipa kodi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga imetoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara katika maeneo yenye  mikusanyiko ya watu, ili wafike kwenye Mamlaka hiyo kufanyiwa makadirio ya kodi mapato ya biashara zao kabla ya tarehe 31 Machi mwaka huu pamoja na kulipa mapato ya awamu ya kwanza.

Elimu hiyo imetolewa leo Machi 16, 2023 katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwamo Stendi za Mabasi, Masoko pamoja na Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.

Afisa elimu mlipa kodi kutoka TRA mkoani Shinyanga Semeni Mbeshi, amewataka wafanyabiashara mkoani humo, wafike kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo ili wakakadiriwe kodi ya mapato ya biashara zao pamoja na kuanza kulipa mapato kodi ya awamu ya kwanza, fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo kuwaboreshea mazingira rafiki ya kufanyabiashara zao.

“Tunawaomba Wafanyabiashara mfike kwenye Ofisi zetu za TRA kwa ajili ya kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato ya biashara zenu ili mlipe mapato kabla ya Machi 31 mwaka huu pamoja na kulipa kodi ya awamu ya kwanza,”amesema Semeni.

“Faida ya kulipa kodi kwanza utafanya biashara zako kwa uhuru, pamoja na kuchangia mapato ya Serikali, fedha ambazo zitarudi kwenu na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo,” ameongeza Semeni.

Nao baadhi ya wafanyabiashara akiwamo Mussa Kubilu wameishukuru TRA kwa kuwakumbusha kulipa kodi kwa hiari yao wenyewe, huku wakitoa wito kwa Mamlaka hiyo iendelee kudai kodi kwa njia Rafiki.
Afisa elimu mlipakodi kutoka TRA mkoani Shinyanga Semeni Mbeshi akitoa elimu ya mlipa kodi na kuwataka wafanyabiashara wafike kwenye Ofisi za TRA ili wakafanyiwe makadirio ya kodi ya mapato ya biashara zao kabla ya Tarehe 31 Machi mwaka huu.
Afisa elimu mlipakodi kutoka TRA mkoani Shinyanga Semeni Mbeshi akitoa elimu ya mlipa kodi na kuwataka wafanyabiashara wafike kwenye Ofisi za TRA ili wakafanyiwe makadirio ya kodi ya mapato ya biashara zao kabla ya Tarehe 31 Machi mwaka huu na kuanza kulipa kodi ya awamu ya kwanza.
Elimu ya mlipakodi ikiendelea kutolewa.
Elimu ya mlipakodi ikiendelea kutolewa.
Afisa kodi kutoka TRA mkoani Shinyanga Deogratius Kyungay akitoa elimu ya mlipakodi na kuwataka wafanyabiashara wafike kwenye Ofisi za TRA ili wakafanyiwe makadirio ya kodi ya mapato ya biashara zao kabla ya Tarehe 31 Machi mwaka huu na kuanza kulipa kodi ya awamu ya kwanza.
Elimu ya mlipa kodi ikiendelea kutolewa.
Wananchi wakisikiliza elimu ya mlipa kodi kutoka kwa Maafisa wa TRA.
Elimu ya mlipa kodi ikiendelea kusikilizwa.

Wananchi wakijibu maswali ambayo walikuwa wakiulizwa mara baada ya kumaliza kupewa elimu ya ulipaji kodi.

Wananchi ambao wamekuwa wakipatia maswali ya ulipaji kodi wakipewa zawadi.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa wananchi ambao wamekuwa wakijibu maswali vizuri ya ulipaji kodi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم