WATUMISHI VETA SHINYANGA WAPEWA SEMINA KUHUSU MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA...WAKUMBUSHWA KULINDA AFYA ZAO

Watumishi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoani Shinyanga wakiwa katika Semina ya utumishi wa umma na kuzingatia afya zao wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WATUMISHI wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Shinyanga, wamepewa elimu ya maadili ya utumishi wa umma, kwa kuzingatia kanuni Nane ili wawajibike vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Elimu hiyo imetolewa leo Machi 16, 2023 kwenye kumbi za mikutano katika Chuo cha VETA Shinyanga.

Afisa Maadili Mwandamizi Vupala Mbwilo kutoka Ofisi ya Rais Sektretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, akitoa elimu ya maadili ya utumishi wa Umma kwa watumishi wa VETA, amewataka wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao muda wote wazingatie maadili hayo ili wafikie malengo yao na kufanya kazi kwa ufanisi.

“Watumishi wa VETA muda wote mnapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yenu, zingatieni kanuni Nane za maadili ya utumishi wa Umma ili mfanye kazi kwa ufanisi,”amesema Mbwilo.

Aidha, amezitaja kanuni hizo Nane za maadili ya utumishi wa Umma ambazo watumishi hao wa VETA wanapaswa kuzizingatia, kuwa ni kutoa huduma bora, kufanya kazi kwa bidii, kutoa huduma bila upendeleo, kufanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji kwa umma, kuheshimu sheria, kutii Serikali na matumizi sahihi ya taarifa.

Naye Afisa Maadili Onesmo Msalangi, amesema uzingatiaji maadili ni muhimu sana katika utumishi wa umma, na kuwataka watumishi hao wa VETA mafunzo ambayo wamewapatia wayashike na kuyatekeleza kwa vitendo.

Kwa upandewake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. Zizima Mohamed, awali akitoa elimu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, amewataka watumishi hao wa VETA wanapokuwa katika majukumu yao wazingatie pia suala la afya zao kwa kufuata ratiba ya kula chakula, kufanya mazoezi pamoja na kupima afya mara kwa mara.

Nao baadhi ya watumishi VETA wameshukuru kupewa elimu hiyo, ambayo wamesema itawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha, katika semina hayo zimewasilishwa mada Saba ikiwamo ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Maadili katika Sekta ya Umma, uwajibikaji wa pamoja katika Sekta ya Umma, ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma, udhibiti wa mgongano wa maslahi,maadili katika jamii, na mwongozo wa mavazi kwa watumishi wa umma.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele akizungumza kwenye Semina hiyo.
Daktari wa Magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk. Zizima Mohamedi akitoa elimu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa watumishi wa VETA Mkoa wa Shinyanga.
Afisa maadili mwandamizi Vupala Mbwilo kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kutoka Kanda ya Magharibi Tabora akitoa mada kwa watumishi wa VETA Shinyanga kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.

Afisa maadili Onesmo Msalangi kutoka Ofisi ya Rais Sekretariet ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Magharibi akitoa mada ya elimu ya uwajibikaji katika Sekta ya umma kwa watumishi wa VETA Shinyanga.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoani Shinyanga Magu Mabelele (kulia) akiwa na wawezesha kwenye Semina hiyo kutoka Ofisi ya Rais Sekretariet ya maadili ya viongozi wa umma.
Watumishi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Semina.
Watumishi wa VETA Shinyanga wakiendelea na Semina.

Washiriki wakiuliza maswali kwenye Semina hiyo.
Maswali yakiendelea kuulizwa kwenye Semina hiyo.

Washiriki wakiwa kwenye Semina.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya Semina kumalizika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments