AJALI YAUA ASKARI POLISI PWANI



Watu watatu wamekufa wakiwemo askari polisi wawili na karani wa mahakakama, huku askari mwingine akijeruhiwa, baada ya gari ndogo waliokua wakisafiria kuacha njia na kugonga karavati kisha kupinduka.


Ajali hiyo imetokea leo Machi 5, 2023 saa 11:45 Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga barabara kuu ya Chalinze – Segera mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea tukio hilo na kutaja gari hilo lenye namba T.323 BAL aina ya Toyota Crester likiendeshwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ndwanga Danstan (28) wakitokea Chalinze kuelekea Lugoba.


“Ni kweli tumepoteza askari wetu wawili na mmoja majeruhi baada ya gari wlailokuwemo kuacha njia kutoka upande wa kushoto wa barabara na kwenda upande wa kulia na kugonga kalavati na kisha kupinduka.

“Ajali imesababisha vifo vya watu wa tatu na majeruhi mmoja na uharibifu wa gari hilo," amesema Lutumo.

Amewataja waliofariki kuwa ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28) aliyekuwa dereva wa gari, Polisi Konstebo Emiliana Charles (26).


Amemtaja mwingine aliyefariki kuwa ni Karimu Simba (27) aliyekuwa karani wa Mahakama ya Wilaya ya Lugoba.

Aidha majeruhi wa ajali hiyo ametajwa kuwa ni Polisi Konstebo Mwanaidi Shabani (25) aliyeumia maneneo mbalimbali ya mwili wake na amepelekwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.


Kwa mujibu wa RPC Lutumo, uchunguzi wa awali umeweza kubaini, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari hilo.


Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Lugoba Chalinze ikisubiri taratibu zingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments