MBUNIFU WA MAVAZI NCHINI KASIKANA AJA NA JUKWAA LA KUTANGAZA WABUNIFU MIKOA YA KANDA YA ZIWA



Mbunifu wa mitindo ya mavazi Kutoka Mkoani Geita, Bertha Joseph Komba(KASIKANA) anatarajia kuzindua Jukwaa la Golden Fashion Festival ambalo linalengo la kuibua vipaji mbali mbali vya wabunifu pamoja na kuhimiza jamii kuipa thamani biashara ya ubunifu kwani bado jamii kubwa hapa nchini imekuwa ikipuuzia kazi mitindo hasa ushonaji kwa kuona kazi hiyo aina manufaa makubwa.


Akizungumza na waandishi wa mbunifu wa mavazi Bertha Komba almaarufu Kasikana Collectione amesema ameamua kuja na jukwaa la Golden Fashion Festival kwa lengo la kuibua na kutangaza vipaji vya wabunifu kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na kuipa thamani kazi ya ubunifu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikikosa sapoti kutokana na kuonekana ni kazi ya maslahi kidogo.

“Tuna imani kupitia jukwaa hili tutaiomba Serikali kuitazama kwa jicho la kipekee Sanaa ya ushonaji na ubunifu kwa waweze kuiongezea thamani hasa katika matumizi yam ashine za kisasa ,lakini pia iweze kuboresha vyuo vya ufundi na kujenga viwanda vya ushonaji ambavyo vitasaidia vijana wengi kupata ajira”, ameeleza Kasikana.


Kasikana ameongeza kuwa ni vyema kwa Watanzania wakapenda vitu vinavyotengenezwa Nchini ikiwa ni pamoja na kuwatumia wabunifu mbali mbali nguo au vitu ambavyo wanaviitaji na kwamba matarajio ya jukwaa hilo ni kuwafikia wabunifu waliopo Kwenye Wilaya tano zilizopo Mkoani Geita pamoja na ambao wapo vijijini ambao bado awajapata nafasi ya Kutangaza vitu ambavyo wanabuni.


“Hivyo natangaza rasmi kwamba natarajia Kutambulisha jukwaa hili na kuzindua ifikapo tarehe 3/3/2023 kwenye ukumbi wa Otonde Plaza ndani ya uzinduzi natarajia kuonesha ubunifu wangu na kuwatambulisha baadhi ya wanamitindo ambao watakuwa wamevaa mavazi yaliyobuniwa”, amesema Kasikana.


“Pia kutakuwa na mavazi ambayo yatauzwa hapo hapo. mara bada ya uzinduzi na utambulisho wa jukwaa hili tutaanza mchakato wa maandalizi ya Tamasha kubwa la mitindo ambalo tunatarajia kulifanya mwezi wa12 mwaka huu”, amesema Kasikana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments