RC NAWANDA AONGOZA KIKAO CHA RCC SHINYANGA, AWA WA MOTO BALAA WANAFUNZI 2344 KUBAKI MTAANI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda akizungumza kwenye kikao cha RCC.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yahaya Nawanda, ameongoza kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) na kueleza kutoridhishwa na hatua ambayo inaendelea ya kuripoti shule kwa wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Kikao hicho kimefanyika leo Februari 14, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama na Wabunge.

Nawanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, amesema bado hajaridhishwa na kasi ya wanafunzi kuripoti shule ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, na kuwaagiza Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Maofisa elimu na watendaji wote wa Serikali hadi kufikia Jumatano ijayo wanafunzi 2344 ambao hado wajaripoti shule, wote wawe shuleni.

“Kikao kilichopita nilikuta asilimia 60 tu ya wanafunzi ambao wameripoti shule kuanza kidato cha kwanza nikatoa maagizo sasa imefikia asilimia 93 bado asilimia 7 hivyo hadi kufikia wiki ijayo nataka nipate taarifa hakuna mwanafunzi ambaye hajaripoti shule awe na sare asiwe na sare wote wawe shuleni,”amesema Dk. Nawanda.

“Kama zoezi hili limewashinda Wakuu wangu wa wilaya niambieni niingie mwenyewe mitaani kusaka watoto wote ambao bado hawajaripoti shule, lakini najua hili haliwezi kuwashinda na imani hadi kufikia wiki ijayo nitapewa taarifa wanafunzi wote 2344 ambao walisalia kuripoti shule watakuwa shuleni,”ameongeza.

Akizungumzia suala la kilimo amewataka viongozi kuhimiza wananchi kuhifadhi chakula ambacho watafanikiwa kuvuna, pamoja na Maofisa Ugani kutoa elimu kwa wakulima kuzitumia mvua chache ambazo bado zipo kwa kulima mazao yanayostahimili ukame.

Amegusia pia suala la kampeni ya upandaji miti na kutoa wito kwa wananchi waendelee kupanda miti kwa wingi ili kuifanya Shinyanga iwe ya kijani pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha, Nawanda katika kikao hicho amewataka pia viongozi wa we wabunifu katika utendaji wao kazi, pamoja na kuwa na utamaduni wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwamo na Migogoro ya Ardhi.

Pia amemuahidi Rais Samia pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, kuwa ataendelea kuzisimamia vizuri fedha za miradi za maendeleo ambao zimekuwa zikitolewa na Rais na kutekeleza madhumuni yaliyokusudiwa na kujengwa kwa kiwango kikubwa.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, Awali akizungumza kwenye kikao hicho, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi mkoani humo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwataka viongozi kuwa fedha ambazo zinaendelea kuletwa wazisimamie vizuri na siyo kuzichezea.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza kwenye kikao hicho amepongeza mapinduzi makubwa ya maendeleo ambayo yamefanywa na Rais Samia katika Mkoa wa Shinyanga.

Katika kikao hicho zimewasilishwa taarifa mbalimbali pamoja na kujadiliwa zikiwamo Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Umeme , Madini na Taarifa ya Benki kuu na Sensa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye kikao cha RCC.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, akizungumza kwenye kikao cha RCC.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye kikao cha RCC.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao cha RCC.

Wabunge wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha RCC.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akiwa kwenye kikao cha RCC.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Kikao cha RCC kikiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Kikao cha RRC kikiendelea.

Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava akiwa kwenye kikao cha RCC.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Kikao cha RCC kikiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Kikao cha RCC kikiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa wa Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments