WAHUNI WAMVAMIA KAMANDA WA POLISI, WAPORA REDIO NA BUNDUKI

Polisi katika kaunti ya Busia nchini Kenya wanatafuta bunduki iliyoibwa kutoka kwa kamanda wa polisi usiku wa Jumamosi, Februari 18,2023.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wezi walivunja nyumba ya kamanda huyo na kuichakura kabla ya kuiba redio na bastola yake aina ya Czeska.

Wezi hao pia walivamia nyumba ya wafanyakazi wake na kuiba mtungi wa gesi na redio.

 Polisi pia wanashuku kuwa wezi hao walinyunyiza dawa ya kulewesha kupitia kwa dirisha la chumba cha kulala ambacho kilikuwa wazi huku kamanda huyo akilalamikia kuwa na maumivu ya kichwa na kizunguzungu alipoamka.

"Iliripotiwa na Kamanda wa CIPU wa kaunti hiyo ya Busia, Bishar Muhumed SSP kwamba jana mwendo wa saa 9.30 usiku, alifunga nyumba yake katika makao ya serikali, Milimani Estate iliyoko takriban mita 300 kutoka mpakani na kulala," taarifa hiyo ya polisi ilisoma kwa sehemu. 

"Leo mwendo wa saa 0335 aliamka akihisi maumivu ya kichwa na kizunguzungu baada ya kuona sanduku lake limetupwa chini karibu na kitanda chake huku nguo zikiwa zimetawanyika kote. Bastola yake ya Czeska Pistol no.F8457 ikiwa na risasi 15 kwenye koti moja haipo," taarifa imeongezwa.

Maafisa wa usalama wa eneo hilo walitembelea eneo la tukio na kikosi cha wapelelezi. "Mbwa wa kundi la K9 aliletwa kwenye eneo la tukio na kuchukua harufu ambayo ilitupeleka kwenye barabara inayoelekea Uganda lakini harufu ilitoweka kabla ya kufika kwenye mpaka. Kikosi cha maafisa wa polisi walivamia eneo hilo ili kupata bunduki hiyo. Hakuna aliyekamatwa au kupatikana hadi sasa,” iliongeza taarifa hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments