NECTA YASITISHA UTARATIBU WA KUTANGAZA SHULE BORA/MWANAFUNZI BORA MATOKEO KIDATO CHA NNE


Baraza la mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne 

Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani Tanzania NECTA Athumani Salumu Amasi amesema utaratibu huo wa kutangaza shule bora ulikuwa unazitangazia biashara baadhi ya shule.

"Kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia Marketing kwa kuitaja tu hiyo shule, shule zipo nyingi zaidi ya elfu 18, sasa unapotaja moja sidhani kama ina tija" amesema Athumani Salumu 

Kuhusu kumtangaza mwanafunzi bora wa mtihani huo amesema hakuna tija katika hilo kwani hauwezi kumtangaza mwanafunzi mmoja katika ya wanafunzi wote Tanzania ambao huenda pia mazingira yao ya kusoma yalikuwa tofauti 

"Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja" amesema Athumani Salumu 




CHANZO ; EastAfricaTV 





MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) NA MAARIFA (QT) 2022, YAMETANGAZWA RASMI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments