RC SOPHIA MJEMA ATEULIWA KUWA KATIBU ITIKADI NA UENEZI WA CCM, ACHUKUA MIKOBA YA SHAKA

Sophia Mjema
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023.

Baada ya baada ya kikao hicho maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka ametoa taarifa akisema mwaka 2022 CCM ilikuwa na uchaguzi wa chama ngazi ya shina mpaka taifa na baada ya kumaliza kikao hicho wajumbe sita wamechaguliwa ambapo watatu wanatoka Tanzania Bara na watatu Zanzibar ili kukamilisha wajumbe wa kamati kuu kufika 24 ambapo  hao saba kwa mujibu wa katiba wamechaguliwa na safu.

Amewataja wajumbe kutoka Tanzania Bara kuwa ni pamoja na Mizengo Pinda (Waziri Mkuu mstaafu), Hassan Wakasuvi (Mwenyekiti CCM Tabora), Halima Mamuya ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ni Mohamed Abood Mohamed, Injinia Nasri Ally na Leyla Burhan Ngozi.

Shaka amesema kikao hicho kimeithibitisha sekretariet ya Halmashauri kuu ya taifa na kutaja orodha ya wajumbe waliochaguliwa ambapo nafasi ya Katibu Mkuu ameendelea Daniel Chongolo, Naibu Katibu Mkuu Bara Annamringi Macha, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mohamed Said Dimwa.


Amesema nafasi yake ya Katibu Itikadi na Uenezi imechukuliwa na Sophia Edward Mjema ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dk Frank Hawasi, Katibu siasa na uhusiano wa kimataifa Mbarouk Nassoro na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Usi Gavu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments