MFANYABIASHARA AFARIKI AKIMUNG'UNYA URODA NA MREMBO GESTI


Mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 25, amepatikana amefariki dunia katika chumba cha hoteli alichokuwa amekodisha kumumunya urojo na mpenziwe.

Ali Musstafa anaripotiwa kuanguka na kukata roho katika Hoteli ya Avenue Lodge mjini Arua, Uganda kutokana na kushindwa kupumua alikokuwa akirusha roho na mpenzi wake.

 “Mwathiriwa alianguka na kufia chumbani. Mpenziwe alienda na kuwajulisha wasimamizi wa hoteli ambao mara moja walitoa taarifa kwa polisi wa Arua. Eneo la tukio lilikaguliwa na kuhifadhiwa vizuri," ilisoma ripoti ya polisi.

Polisi katika Wilaya ya Arua eneo la Nile Magharibi walisema hawakupata dalili zozote za sumu, dawa za kulevya au athari zingine za mwili kutoka eneo la tukio.

"Hakuna chembechembe za matumizi mabaya ya dawa za kulevya, sumu au athari zingine za mwili zilizopatikana katika eneo la tukio.

 Mwili huo ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Arua na kuchunguzwa,” msemaji wa polisi, SCP Fred Enanga alisema Jumatatu, kama alivyonukuliwa na Daily Monitor.

Enanga anaamini kuwa mfanyabiashara huyo kutoka OZU, wadi ya Kenya katika Wilaya ya Arua alifariki dunia mwendo wa saa tatu usiku. 

Mwili wa marehemu baadaye ulichukuliwa kutoka chumba cha hoteli na kupelekwa kufanyiwa uchunguzi wa maiti.

 "Kifo wakati wa kujamiana kinaweza kutokea kwa sababu kadhaa, ambazo ni pamoja na mkazo wa mwili kutokana na shughuli hiyo au kwa sababu ya hali isiyo ya kawaida ," aliongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments