MWAMBA AFICHUA ANAVYOCHEMSHA NGUO ZA NDANI KWENYE MASHINE YA KUPASHIA CHAKULA KABLA YA KUZIVAA



Mwanaume mmoja amezua gumzo kwenye mtandao wa kijamii baada ya kufichua mtindo wake wa ajabu wa maisha.

Kupitia kitandazi chake cha Twitter chenye jina @samaoxcx, alifichua kwamba huweka chupi zake kwenye mashine ya kupasha chakula (kikangazi) kabla ya kuzivaa kila siku.

Ufichuzi wake ni kutokana na swali kwenye mtandao uliowataka wanamtandao kushiriki mambo ya ajabu kuwahusu ambayo watu wengine hawafahamu. 

Ni kutokana na swali hilo ndipo mwanaume huyo alishiriki picha akisema anapenda kuweka nguo zake za ndani kwenye kikangazi kwa sababu anapenda joto na hisia za mchanganyiko anazopata baada ya kuzivaa.

"Kabla ya kuvaa chupi yangu huwa naziweka kwenye microwave ili ziwe na joto",aliandika.

Twiti yake imezua mjadala moto wengi wakiwa na maswali tumbu nzima wakitaka kujua zaidi kuhusu mtindo wake wa ajabu.

 Huku baadhi wakishangaa kwa nini anaweka chupi yake kwenye mashine ya kupasha chakula, wengine walishangaa iwapo wa ni salama kwa uume wake.

 @sephorajoonie aliandika: "Hakikisha kumwambia bibi unafanya hivyo kabla hajajaribu kupasha moto chakula kwa ajili ya familia kwenye microwave"

 @lvns_svnl aliandika: "Je, hiyo ni nzuri kwa eneo lako la kibinafsi?"

 @Crissasje: "Katika mikrowevu ile ile unatumia kwa chakula!?"

 @B3tterAng3ls aliandika:"Unajua, ningehukumu kwa hili lakini nilifikiria juu yake kwa sekunde. Ni hisia zile zile za kupata blanketi safi kutoka kwenye kifaa cha kukaushia, ili nipate, lakini bado nitahoji hili "

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments