AMCHINJA NA KUMTUPA MTONI MKEWE AKIMTUHUMU KUCHEPUKA


Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia, Mapinduzi Siliya (45) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Terezia Mtajiha.


Siliya anadaiwa kumchinja kwa kutumia kisu kisha mwili kuutupa mto Nzovwe jijini Mbeya.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Januari 11, 2022 na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kwa uchunguzi wa kitabibu.


Kuzaga amesema kisa cha mauaji hayo ni mtuhumiwa kumtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments