TBS YAKABIDHI LESENI NA VYETI 59 KWA WAZALISHAJI WA BIDHAA MKOANI MBEYA


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekabidhi Leseni na Vyeti vya ubora hamsini na tisa (59) na kati ya hivyo, leseni na vyeti 39 (66.1%) vimetolewa kwa wajasiriamali wadogo ambapo leseni na vyeti hivyo vimetolewa kwa wazalishajiwa bidhaa ambazo zimekidhi viwango.

Vyeti na leseni hizo ni kwa ajili ya bidhaa za vyakula, vipodozi, vifaa vya ujenzi, chaki, gesi, makaa ya mawe na vifungashio.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo iliyofanyika leo Desemba 16,2022 mkoani Mbeya, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mwajuma Nyamkomola amesema

Aidha amesema serikali imekuwa ikiwahudumia wajasiriamali wadogo katika kupata huduma za TBS bila malipo na gharama za ukaguzi na upimaji kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ya mwanzo.

"Naipongeza Serikali kwa kuendelea kutambua uhitaji wa kuendelea kuwalipia wajasiriamali wadogo hata baada ya kipindi cha miaka mitatu kwisha kutokana na hali ngumu ya biashara inayosababisha kutofikia uwezo wa kuanza kujilipia. Hatua hii inasaidia katika kuinua na kukuza viwanda hapa nchini". Amesema

Amesema serikali za Mkoa na Halmashauri wanaendelea kushirikiana na taasisi wezeshi ikiwemo TBS kuhakikisha wanakua kuanzia kuwa na bidhaa zenye viwango ili kupata soko kiurahisi na kumudu ushindani.

Ameipongeza TBS kwa kufanya hafla hizo katika Kanda zake kwa kuanzia katika mkoa wangu wa Mbeya. Kwa niaba ya mikoa ya wenzangu, naamini fursa hii ya kufanyika hafla katika mikoa italeta hamasa na chachu ya wazalishaji Zaidi ya waliohudhuria hapa, kuzalisha bidhaa zenye ubora na bila shaka wataongezeka katika kuomba kuthibitisha bidhaa zao kwa TBS.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa wazalishaji wote ambao hawajapata leseni na vyeti vya ubora walioko katika mikoa ya Kanda za Nyanza za Juu Kusini na Magharibi mwa Tanzania ambako ofisi za TBS zipo, waendelee kufuata taratibu za shirika ili nao waweze kupata alama za ubora kwa ajili ya usalama wa mlaji na kuyafikia masoko ya ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo amewahasa waliopata leseni na vyeti vya ubora kuwa muwe mabalozi wazuri katika matumizi ya Viwango ili kufikia lengo la Tanzania ya viwanda na muendelee kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya Viwango kwa mustakabali wa afya za watumiaji na kukuza soko la ndani na nje ya nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments