KLABU YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA YAENDESHA MKUTANO MKUU MAALUM, SATURA AVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KUCHOCHEA MAENDELEO



Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura akizungumza kwenye Mkutano huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KLABU ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) imeendesha Mkutano Mkuu maalum wa kujadili maendeleo ya Klabu hiyo pamoja na kupitia maazimio 10 ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) uliofanyika Desemba 6 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo Mkuu maalum wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, umefanyika leo Desemba 20, 2022 na kuhudhuriwa na wanachama wa klabu hiyo, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula, akisoma taarifa ya klabu hiyo kwenye Mkutano huo Maalum, amesema wana jumla ya wanachama 35, wanaume 22 na wanawake 13.

Amesema lengo la mkutano huo maalum ni kujadili maendeleo ya klabu kutokana na mpango mkakati mpya wa “From Good to Great” yaani kutoka kwenye maendeleo makubwa kwenda makubwa zaidi, chini Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC­).

“Mpango Mkakati wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) wa “From Good to Great” unalenga kukuza mahusiano na wadau, kuongeza wanachama wa klabu, na kukuza Tasnia ya habari, na klabu kuweza kujitegemea,” amesema Mabula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura, akizungumza kwenye mkutano huo, amesema Serikali inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhabarisha umma pamoja na kuchochea maendeleo.

Amesema Ofisi yake ipo tayari kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika nyanja mbalimbali, ikiwamo na kutangaza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetekelezwa na inayoendelea kutekelezwa pamoja na vivutio vya utalii vilivyopo manispaa ya Shinyanga.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Patrick Mabula, akisoma taarifa ya Klabu kwenye Mkutano huo.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Estomine Henry akisoma Maazimio 10 ya Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa wanachama wa Shinyanga Press Klabu kwenye mkutano huo.

Waandishi wa habari ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga SPC wakiwa kwenye Mkutano Maalum.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Mkutano Mkuu Maalum ukiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye mkutano huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments